Korea Kaskazini Yaonywa na Baraza la Usalama la UN

 Korea Kaskazini Yaonywa na Baraza la Usalama la UN
Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limelaani kitendo cha Korea Kaskazini cha kurusha kombora kupitia anga ya Japan, huku nchi hiyo ikithibitisha kutekeleza.

Taarifa iliyoandikwa na Marekani, haikutishia kuiwekea vikwazo vipya Korea kaskazini.
Lakini Baraza la Usalama limeitaka Korea Kaskazini kusitisha majaribio zaidi na kusitisha mpango wake wa nuklia.

Wanachama 15 wa Baraza hilo la Usalama wameitaka Korea Kaskazini kuchukua hatua za haraka kupunguza hali ya wasiwasi uliyopo.
Majeshi ya Korea Kusini na Marekani yamekuwa yakifanya mazoezi ya pamoja karibu na mpaka wa Korea Kaskazini, jambo ambalo Pyongyang inasema ni mazoezi yenye kulenga uvamizi wa kijeshi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad