Kutana na Muuza Maji ya Madumu Anayetengeneza Pesa Nyingi Kwa Mwezi zaidi ya mtu Mwenye Degree.

Salaam wakuu,
Siku chache tu zilizopita, nilihamisha makazi yangu kutoka Sinza na kuhamia magomeni makanya.

Hapa pana shida ya maji sana. Sasa kuna kijana mmoja wa kisukuma almaharufu kwa jina la Ngosha, anauza maji ya madumu kwa ajili ya matumizi. Dumu moja anauza Shilingi 500.

Ana jumla ya madumu 50. Huamka asubuhi na mapema sana majira ya saa kumi. Huyafuata maji na mkokoteni wake hadi majira ya saa moja, anakua amejaza madumu yote 50 na kuyaleta makanya kuyauza.

Ikifika mida ya saa nane mchana, hua anakua ameuza madumu karibu 40, hivyo anafuata madumu mengine kama 20 hivi kwa ajili ya kuuza jioni. Anauza maji hadi saa tano usiku. Kuna wakati ikifika mida ya saa tatu usiku, anakuwa amemaliza maji na anakwenda kupumzika.

Nilimuuliza siku biashara ikiwa mbaya, anakuwa ameuza madumu mangapi, akaniambia 50. Sasa tuchukue hii minimum tuifanye ndo kwa kila siku, kwa mwezi inakuwa ni pesa nyingi zaidi ya hata mtu anayelipwa mshahara wa degree.

Chukua 50x500= 25,000. Alafu chukua 25000x30=750,000.
Kwahiyo huyo kijana anapata shilingi laki saba na nusu kwa mwezi ambayo hata hatozwi kodi.. Hiyo ni take home.

Huyu kijana maisha yake ni mazuri, ana mke na watoto wawili. Amekodi vyumba vitatu kwa ajili ya kuishi yeye na familia yake. Mtoto wake wa kwanza yupo darasa la kwanza.

Asubuhi anapata breakfast nzito ambayo ni chapati mbili, maharage bakuli moja, supu ya utumbo bakuli moja, soda moja ya pepsi na maji ya masafi lita moja. Hiyo ni asubuhi tu. Jioni lazima apate bia mbili pia.

Kwa sasa amenunua kiwanja huko mbezi na anajenga nyumba yenye Rumu nne.
Huyu kijana hata mimi mshahara wangu ni mdogo zaid ya anachoingiza.
Kweli kusoma siyo kupata pesa mingi na kufanikiwa.

Wakati huo huo mimi ninawaza hapa napata wapi hela ya kodi mwezi ujao landlord ameanza kukumbusha...
Ngoja nipate chai ya Tangawizi +asali +mdalasini.. Then narudi.

Imeandikwa na Mjina Mrefu
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Wacheni uhasidi nyinyi Tafuteni na nyinyi riziki.
    mpaka chakula anachokula unatangaza.sasa TRA WAMFATE ALIPE KODI ya mapato?
    anatumia mwili wake kusukuma mikokoteni yenye madumu 50.sio pick up ni binadamu huyo
    Abarikiwe na MUNGU

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad