Kwanini Roma Mkatoliki Anakataa Kabisa Kusema Alihojiwa nini na Watekaji?

Nimemsikiliza Roma Mkatoliki akihojiwa na Millard Ago kwa takribani dakika 35 lakini amekataa kata kata kueleza alikuwa anahojiwa nini!

Ameeleza tukio zima la yeye na Monie,Bin laden na Imma kuchukuliwa studio mpaka huko wasikokujua.

Ameeleza mateso aliyoyapata mpaka kuvunjwa kidole cha mwisho mkono wa kushoto na kuvunjwa jino la juu kwa kupigwa na mijeledi,virungu huku wakiwa wamefungwa USO na mikono na mateke huku mdomo Umefungwa sole tap usije ukatoa sauti

Roma alikuwa room ya peke yake,Imma room ya peke yake na Monie na Bin laden walikuwa room ya peke yao.

Na aliambiwa atatoka mwaka 2030 kama wimbo wake alioimba Roma.

Swali langu kwanini Roma anakataa kabisa na hata Katika hayo mahojiano kueleza alihojiwa nini?!

Ila anachosisitiza hayo yote aliyoulizwa yeye hayafanyi na anamwachia Mungu.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad