Malinzi na Wenzake Mambo Bado Magumu Mahakamani

Malinzi na Wenzake Mambo Bado Magumu Mahakamani
KISUTU leo upande wa utetezi katika kesi inayomkabili aliyekuwa Rais wa TFF, Jamal Malinzi na wenzake umeiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kutoa maelekezo mahususi kwa upande Serikali kuharakisha upelelezi dhidi ya washitakiwa, kinyume na hapo Mahakama iwasikilize na iwaachiwe huru.

Akiieleza mahakama hiyo wakili wa utetezi, Domician Rwegoshora amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri kwamba wanautaka upande wa mashtaka uharakishe upelelezi kwa sababu kesi hiyo haina dhamana, hivyo washtakiwa wakiendelea kukaa ndani wanateseka.

”Naiomba Mahakama itoe maelezo mahususi kwa upande wa mashtaka kwa muda mfupi, au washtakiwa wasikilizwe ikiwezekana Mahakama iwaachie.” alisema Domician.
Baada ya kueleza hayo, Wakili wa Serikali, Vitalis Piter akaeleza kuwa upelelezi upo katika hatua ya mwisho na muda si mrefu itaanza kusikilizwa.

Naye Hakimu Mashauri ameahirisha kesi hiyo hadi Septemba 9, mwaka huku akiutaka upande wa Serikali kuharakisha na ikiwezekana katika tarehe hiyo watoe taarifa kuhusu upelelezi ulipofikia.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad