Serikali ilisema mazishi ya pamoja yangeahirishwa hadi leo ili kutoa fursa kwa ndugu na jamaa kutambua miili ya maiti ya waathirika.
Lakini mkuu wa wataalamu wa magonjwa kutoka mjini Freetown ameiambia BBC kwamba baadhi ya mazishi yalikuwa yamefanyika.
Imefahamika kuwa mazishi hayo yamehusisha miili ambayo tayari ilitambuliwa au ilikuwa imeharibika kabisa.
Nathaniel Williams ni daktari katika hospitali kuu ya Connaught, iliyopo Freetown, anasema hivi sasa kuna tahadhari kubwa ya kutokea magonjwa ya milipuko kama vile kipindupindu.
Ameongeza kusema kuwa hivi sasa kunahitajika madawa na vyakula, kwa wale walioathirika.
Hata hivyo, Umoja wa Mataifa nchini humo umesema tayari umeweka mikakati ya kuweza kukabiliana na magonjwa ya milipuko iwapo yatatokea.