MAN WATER: WCB Kutoa nyimbo Baada ya Ali Kiba Watapotea Tuu

MAN WATER: WCB Kutoa nyimbo Baada ya Ali Kiba Watapotea Tuu
Producer wa ‘Seduce Me’ Man  amezungumzia ishu ya wasanii kuachia wimbo baada ya saa chache msanii mwingine kuachia wimbo mda mchache na kusema lazima wasanii wanapoachia nyimbo zao lazima wapeane nafasi na kama wimbo uliotoka baada ya Alikiba basi hautadumu kwenye soko, utapotea.

>>>”Wasanii ufike wakati tusifanye kwa ushindani – kama upande mmoja umeshaachia wapeane nafasi kama tunataka kujenga na kutengeneza hits vinginevyo tusipoangalia tutauwa tunaziua na wasanii watapotea kwa haraka sana kwa sababu hazitokuwa kazi zaubunifu bali za kupanic.

“Kama kuna ngoma imetoka katika hali ya ushindani, nina uhakika kwamba asilimia kubwa itapotea. Siitabirii vibaya ila kuna mambo ya kujipanga ili kupeana nafasi.” – Man Water.

Mwimbaji staa wa Bongofleva Alikiba aliachia video ya wimbo wake mpya unaoitwa ‘Seduce Me’ ambao umekuwa gumzo ambapo saa chache baadaye WCB wakiongozwa na Diamond Platnumz waliachia video yao mpya pia ‘Zilipendwa’ kitendo kilichopokelewa kwa hisia tofauti.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad