Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba, Haji Manara amesema kuwa ushindi wao walioupata dhidi ya Yanga SC katika mtanange wa Ngao ya Jamii unatokana na ubora wa kikosi walicho nacho msimu.
Manara amesema, “Timu bora siku zote inashinda haijalishi ni katika mazingira gani lazima ipate ushindi na mipango yetu ilikuwa ni kupata magoli matano kwa mazingira yoyote yale iwe ni penati ama ndani ya dakika 90 ilikuwa lazima yapatikane hivyo tunashukuru ni mwanzo mzuri wa ligi.”
Ameongeza, “Mara ya mwisho niliwaambia Yanga kama waamuzi wakichezesha kwa haki hawatatufunga kokote mechi zote walizoshinda walikuwa wakibebwa kwa hiyo nawaomba shirikisho lampira wa miguu Tanzania (TFF) waendelee kupanga waamuzi bora hata huyu waleo alikuwa na mapungufu lakini ya kwake ni ya kibinadamu kila mtu ameyaona kwa pande zote mbili.”
“Kesho kikosi chetu kitapumzika ila tutaingia kambini jioni kwaajili ya mechi yetu ya Jumamozi dhidi ya Ruvu Shooting tunawashukuru sana wachezaji wetu wamefanya kazi kubwa sana lakini pia wengi bado wapya hivyo mwalimu ataendelea kuiboresha zaidi,” amesema Haji Manara.
ala kumbee,kama kweli vilee,mpira unachezwaga na simba mwisho wa siku inafungwa simba maajabu...magufuli oyeeeeeee
ReplyDeletesasa YANGA kwisha habari yao..no manji no win sawa sawa na rushwa kwa marefarii na wachezaji...marenzimen..MAGUFULI oyeeee,KAPITANYO e CHIDY JEMBE oyeeeeee.
ReplyDelete