Diwani wa Mbagala kwa tiketi ya CCM, Yusuf Manji jana alisema mbele ya mahakama kuwa hataki kuwakilishwa na Wakili Peter Kibatala na kutaka abadilishe wakili kwa kile alichosema kuwa ni kutofautiana kwa itikadi za kisiasa.
Manji ambaye ni mmoja wa wafanyabiashara wakubwa nchini Tanzania aliiambia Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam jana kabla ya kuanza kusikilizwa kwa kwa maombi yake ya dhamana ambapo alishangaa yeye kama Diwani wa CCM kuwakilishwa na wakili ambaye ni mwanachama wa CHADEMA.
Manji anayekabiliwa na tuhuma za uhujumu uchumi, baada ya kumkataa wakili huyo aliwatambulisha mawakili wengine wapya wawili ambao watamuwakilisha.
Aidha, Mahakama Kuu jana ilitupilia mbali maombi ya dhamana ya Manji na kuanza mchakato wa kuipeleka kesi hiyo katika Mahakama Kuu Divisheni ya Uhujumu Uchumi na Rushwa baada ya Manji kukubali pingamizi la Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kuomba kuyaondoa mahakamani maombi ya dhamana.
Mmoja wa mawakili wapya wanaomuwakilisha Manji, Alex Mgongolwa alisema walikubali kuondolewa kwa maombi hayo mahakamani hapo ili kupelekwa katika Mahakama ya Uhujumu Uchumi na Rushwa maarufu Mahakama ya Mafisadi ambayo ndiyo yenye mamlaka ya kusikiliza maombi yao.
Manji anasota rumande kwa siku zaidi ya 30 sasa kutokana na kunyimwa dhamana kila anapofika mahakamani.
Toa Maoni Yako Hapa chini:
Manji Alivyomkataa Wakili wa Chadema Mbele ya Mahakama...Kisa Kizima Hichi Hapa
0
August 09, 2017
Tags