Mapya Yaibuka Sakata la Kusajiliwa kwa Buswita

Mapya Yaibuka Sakata la Kusajiliwa kwa Buswita
Sakata la kiungo wa Yanga SC aliyesajiliwa msimu huu kutoka Mbao FC Pius Buswita kufungiwa mwaka mmoja kucheza mpira lapata sura mpya baada ya katibu mkuu wa Yanga ndugu Charles Boniface Mkwasa kulitolea ufafanuzi.

Buswita amekumbana na rungu la TFF la kutojihusisha na soka kwa mwaka mmoja baada ya kile kinachodaiwa kusajili vilabu viwili kwa wakati mmoja yaani Yanga SC na Simba SC . Simba ndio waliomwekea pingamizi TFF ikidaiwa kawatapeli hivyo kufungiwa mwaka mmoja.

Mkwasa asubuhi ya leo akiongea na kituo cha redio ya EFM amekiri kupokea barua ya hukumu hiyo ikiwaeleza hawataweza kumtumia mchezaji huyo kwa mwaka mmoja kama adhabu yake . Mkwasa amesema kama klabu pia wameiandikia TFF barua kupinga uamuzi huo na kulieleza jambo hilo kwa kina sambamba na maelezo ya mchezaji husika .

” Simba SC wanasema Pius wamemsajili tarehe 2 juni 2017 ilihali kipindi hicho alikuwa ndani ya mkataba na Mbao FC kitu ambacho ni makosa kwa sababu hawakuwafuata Mbao . Sisi tumewafuata Mbao na mchezaji husika na tukamsajili , wakatupa stakabadhi zetu pia release letter kama viambatanisho . Sasa hao Simba walimsajili Pius yupi? ilihali mkataba wake na Mbao umekwisha tarehe 7 August?! Hii ina maana kwanza kabisa Simba ndio wana makosa katika hili kumsajili mchezaji wa watu akiwa ndani ya mkataba bila kuonana na waajili wake. Katika hili Mbao ndio wana haki kuwashitaki Simba ” alieleza Mkwasa.

Mkwasa kaenda mbali kwa kusema waliokuwa wakimrubuni kijana huyu kwa milioni 5 kupitia wazazi wake ni wapenzi wa Simba Mwanza ambao dhamira yao ilikuwa ni kuvuruga usajili huu hivyo TFF walitakiwa kusikiliza pande zote kabla ya kutoa hukumu ( natural justice ) kuliko walivyofanya.

” sisi na Azam tuligongana kwa Hozza wa Mbao lakini mwisho wa siku tukaona isiwe tabu kwa sababu mchezaji husika kaonesha mapenzi ya kwenda Azam , tulipewa pesa zetu na kuliacha suala hilo bila ugomvi , kwanini Simba ?! ” aling’aka Mkwasa.

Sakata hili kuna kila dalili ya taratibu za kiusajili kukiukwa pia hukumu kutoka bila kusikiliza kwa kina pande zote . Hali ambayo imewapelekea Yanga na mchezaji husika kukata rufaa TFF kwa hukumu waliyotoa.

Afisa habari wa Simba SC ameeleza suala la mchezaji huyo wanaweza kulipeleka katika mahakama za kiraia kwa kesi ya utapeli.





Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad