Hii inajiri baada ya baraza la ulinzi la Umoja wa Mataifa, zikiwemo Urusi na China kupiga kura ya kuiwekea viwazo zaidi Korea Kaskazini
Wizara ya fedha nchini Marekani ilisema kuwa vikwazo hivyo vitaongeza shinikizo kwa Korea Kaskazini lakini hatua hiyo imeighadhabisha China
Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Marekani Rex Tilleron, wakati huo huo ameipongeza Korea Kaskazini kwa kujizuia siku za hivi karibuni.
"Hatujashuhudia urushaji wa makombora na vitendo vya uchokozi kutoka Korea Kaskazini tangu azimio la baraza la ulinzi la Umoja wa Mataifa lianze kutekelezwa," alisema.
Wizara ya fedha itaendelea kuongeza shinikizo kwa Korea Kaskazini kwa kuenga wale wanaosaidia kuendelea kwa mipango ya nyuklia na ya makombora ya masafa marefu.
Hatua hiyo inamaanisha kuwa watu nchini Marekani na kampuni za Marekani haziruhusiwi kufanya biashara na kampuni zinazosaidia programu za Korea Kaskazini