Maskini..Mwanaharakati wa Kupambana na Ujangili wa Pembe za Ndovu Tanzania Apigwa Risasi Kadhaa na Kufariki


#TANZIA
DAR: Mwanaharakati wa kupambana na biashara ya Pembe za Ndovu, Wayne Lotter apigwa risasi na kufariki. Alikuwa akishirikiana na Polisi kukamata wawindaji haramu wa Tembo.
Wayne Lotter(51), aliuawa wakati akitoka Uwanja wa Ndege kuelekea nyumbani kwake ambapo gari aliyokuwa amepanda ilizuiwa na gari nyingine na ndipo watu 2 wenye bunduki wakampiga risasi.
Aidha bwana Lotter tangu mwaka 2009 amelikuwa akipokea vitisho vya kuuawa kutoka kwa watu wasiofahamika. Hata hivyo Jeshi la Polisi limeanza uchunguzi wa kuwabaini wahalifu waloliotekeleza mauaji haya..Mungu Ailaze Roho Yake Mahali Pema Peponi... Wote tuseme **AMEN** .
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad