Maskini..Utajiri wa Bilione Dangote Waporomoka zaidi ya Nusu...

Aliko Dangote ana utajiri wa dola za Marekani bilioni 12.2 (trilioni 27), ambaye utajiri wake ni takriban asilimia 3 ya pato la Taifa la Naijeria, unamfanya awe mtu tajiri zaidi barani Afrika kwa urahisi — na ndio bilionea mweusi aliye juu zaidi kwenye orodha ya watu matajiri duniani.

Hii ni taarifa nzuri, lakini hii ni nusu tu ya utajiri aliokuwa nao Dangote mwaka 2014 ambapo hadi mwaka huo ulipoisha, Dangote alikuwa na utajiri wa dola za Marekani bilioni 25 (trilioni 56).

Sehemu kubwa ya utajiri wake (asilimia 90) inatoka kwenye viwanda vyake vya kutengeneza saruji (Dangote Cement), kampuni iliyoorodheshwa kwenye Soko la Hisa nchini Naijeria yenye thamani ya dola za Marekani bilioni 11, sawa na trilioni 24.

Biashara za bilionea Dangote zimesambaa kwenye nchi kadhaa barani Afrika. Anamiliki viwanda vya kutengeneza saruji nchini Zambia, Senegal, Tanzania, na Afrika Kusini.

Dangote, ambaye amekuwa Mkurugenzi Mtendaji na Rais wa kundi la kampuni za Dangote kwa zaidi ya miaka 35 sasa pia ni mtu anayetoa misaada ya kibinadamu. Akiwa ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Misaadaya ya Dangote, anasimamia misaada katika elimu, kilimo na afya ikiwamo msaada wa dola za Marekani 12,000 (takriban shilingi nilioni 27) kwa siku kwa watu wanaokosa huduma muhimu.

“Aliko ni tajiri namba moja barani Afrika, na biashara zake zinachangia kukuza uchumi wa bara zima. Hilo ni jambo zuri, lakini namtambua zaidi kama kiongozi ambaye yupo mstari wa mbele kupunguza tofauti kati ya biashara za watu binafsi na sekta ya afya ya jamii nzima,” aliandika bilionea namba moja duniani, Bill Gates. Bilionea huyo kwenye sekta ya teknolojia almemsifu Dangote kwa mafanikio makubwa aliyochangia kuitoa Naijeria kutoka kwenye orodha ya dunia ya nchi zenye magonjwa ya milipuko kwa juhudi zake za kupambana kutokomeza ugonjwa wa polio.

Mwezi Januari 2016, Dangote na Bill Gates walitoa ahadi ya kutoa dola milioni 100 ili kutokomeza utapiamlo nchini Naijeria, nchi yenye idadi kubwa zaidi ya watu barani Afrika.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad