Freeman Mbowe amesema hayo alipokuwa akizungumza na wakazi wa Machame Uroki katika ziara yake ya jimbo na kusema kuwa Kilimanjaro inakuwa kimaendeleo kutokana na baadhi ya wazee miaka hiyo kupata elimu ya kutosha ambayo ndiyo imekuwa chachu ya maendeleo hayo.
"Sifa kubwa ya kwanza katika taifa hili kuhusu mkoa wa Kilimanjaro ni elimu, wazee wetu walisoma siyo wote ila wachache waliosoma walisoma sana kulinganisha na mikoa mingine kwa hiyo maendeleo ya Kilimanjaro hayategemei CCM, bala maendeleo ya Kilimanjaro yalikuwepo hata kabla ya uhuru watu walisoma siku nyingi na watu walipata imani siku nyingi, sifa hii ni lazima tuirejeshe, tuna shule nyingi lakini shule nyingi ni zile ambazo hazina sifa ya kuitwa shule" alisema Mbowe
Aidha Mbowe aliwataka watu kuwekeza nguvu kubwa kwenye elimu kwa watoto wao kutokana na ukweli kwamba ardhi ya kuweza kuwarishisha watoto kwa sasa haipo Kilimanjaro hivyo wanapaswa kuwekeza zaidi na zaidi kwenye elimu na kusema anatambua kuwa wanafanya hivyo ila bado haitoshi wanapaswa kuongeza nguvu zaidi na zaidi.
Huu si ubinafsi bali ukweli. Watu tuache majungu, tuache siasa. Ukweli ni kwamba, Elimu ni ufunguo wa maisha. Ykupata elimu bora, ukajitambua na kujituma utapata maendeleo. Mikoa mingi elimu tabu. Kuna kelele nyingi za kutaka kujipatia pesa, lakini adabu inayotakiwa ili upate maendeleo ni shida. Pia ukiwa na elimu, ustaarabu pia upo. Wengi wetu yunafikiri pesa ni maendeleo si kweli. Maendeleo yanaendana na elimu bora na ustaarabu wa namna ya pekee. Si wote wenye pesa ni wastaarabu.Kuna adabu hawana na hawajijui.Bila ya adabu ya pekee itokanayo na elimu inakuwa ni vigumu sana hata katika undugu, Hurudisha jamii nyuma kabisa.Elimu inamwezesha mtu kufikiri, kujituma, kujitegemea, kuwa maridadi.Ni elimu ndio inahitajika ili tujikomboe kifikra. Wengi wasiosoma inakuwa shida kutumia akili zao vipasavyo.
ReplyDelete