Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema Amekamatwa na Polisi Kwa Madai ya Kuzidisha Muda wa Mkutano‬

Mbunge wa Arusha mjini Mhe.Godbles Lema amekamatwa na jeshi la polisi mkoani humo kwa madai ya kuzidisha muda katika mkutano wake kwa dakika saba (07).

Polisi wanadai Lema amemaliza mkutano saa 12:7 jioni badala ya saa 12:00 kamili kama ilivyo utaratibu.

Polisi "wamemblock" Lema katika "keepleft" cha mnara wa saa kwa kusimamisha gari mbili (moja mbele na nyingine nyuma), kisha kuingia katika gari ya Lema na kumuelekeza kituo kikuu cha polisi (central).

Hali hii imesababisha foleni kubwa kwenye barabara zinazoingia katikati ya mji.

By Malisa Godlisten
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hivi serikali inafaidika nini kutokana na haya. Na Wananchi mnafikiriaje huu oonezi. Dakika saba mtu unafunguliwa kesi. Hii ni Tanzania au? Hii inashangaza. Kisa cha kunyanyasa watu ni nini. Na CCM inafaidikaje. Na Raisi magufuli yupo kimya. Sijawahi ona hii duniani yote. Hivi Tanzania inabadilika hivi. Mbona aibu.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad