Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema Akamatwa na Polisi

Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema Akamatwa na Polisi
JESHI la Polisi mkoani Arusha limemkamata Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema  kwa madai ya kuzidisha muda wakati akihutubia kwenye mkutano wake na wananchi jana Jumatano, Agosti 23, 2017 jijini humo.

Polisi wamedai kuwa Lema alimaliza mkutano wake saa 12:7 jioni badala ya saa 12:00 kama ilivyo utaratibu.
Hivyo askari polisi walimzuia katika mzunguko wa barabara wa Mnara wa Saa (round about) kwa kusimamisha gari mbili (moja mbele na nyingine nyuma), kisha kuingia katika gari yake na kumuelekeza Kituo Kikuu cha Polisi (Central Police) mjini Arusha.

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. hawa polisi wa Tanzania na serikali yake nikama wandawazimu, vitendo vya kukamatakamata wapinzani kwa sababu za kijinga zinajenga imani mbaya kwa sisi wananchi.eti kazidisha dakika 7 kwenye mkutano wake.that is nonses and wasting time, wanawaonesha nini Watanzania kwasabu zao za kijinga kijinga. au wanataka waonekane wako busy nawao wanafanya kazi ?

    ReplyDelete
  2. hapana kuzingatia wakati ni jambo muhimu.angalia ukienda cyber cafe ukichukua dak 15. hiwa inazidi? Vp goless achukue zaidi..katumwa au hakasoma kibali au ni dharau..lazima tumkumbushe umuhimu na ruhusa izingatiwe. hapa ni kazi tu

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad