Mbunge wa Bunda Ester Bulaya Hali Mbaya Azidiwa Ghafla Rumande

Mbunge wa Bunda Ester Bulaya Hali Mbaya Azidiwa Ghafla Rumande
MBUNGE wa Bunda Mjini, Ester Amos Bulaya (Chadema) amelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Tarime mkoani Mara usiku wa kuamkia leo baada ya kuugua ghafla akiwa rumande ambako alikuwa ameshikiliwa na Jeshi la Polisi Kanda ya Tarime Rorya baada ya kumkamata akiwa hotelini kwa madai ya kutaka kufanya mkusanyiko usio halali.

Taarifa za kulazwa kwa Bulaya zimethibitishwa na Katibu wa Mbunge Tarime Vijijini, John Heche (Chadema), Mrimi Zabron ambaye ameeleza kuwa Bulaya anasumbuliwa na kifua ambacho kimesababisha ashindwe kuzungumza lakini hata hivyo madaktari wanaendelea kumtibu.
Aidha imeelezwa kuwa, Bulaya alianguka na kupoteza fahamu akiwa rumande hivyo kukimbizwa hospitali kwa matibabu.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad