Mfanyabiashara Kizimbani kwa Kukutwa na Sare za JWTZ
0
August 16, 2017
Casto Onyomolile Ngogo (35) mfanyabiashara wa Kariakoo jijini Dar es salaam, amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu shtaka la kukutwa na suruali 5,000 za Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ).
Akisoma hati ya mashtaka, Wakili wa Serikali, Wankyo Simon kwa Hakimu Mkazi Mkuu,Thomas Simba alidai kuwa Ngogo ambaye ni mkazi wa Tabata Segerea, alikutwa na vifaa hivyo katika maeneo ya bandari kavu ya Galco Inland Container (ICD) iliyopo Sokota Chang’ombe Juni 15 mwaka huu .
Wakili wa Serikali, Simon alidai kuwa siku hiyo, mshtakiwa huyo alikutwa na suruali 5,000 za JWTZ zenye thamani ya Shilingi 50 milioni ambazo zimepatikana kwa njia isiyo halali.
Juni 15 mwaka huu, Ngogo anadaiwa kuwa katika eneo hilo alikutwa na maofisa wa Jeshi la Polisi akiwa na tisheti 50 za JWTZ zenye thamani ya Shilingi 500, 000.
Hata hivyo mshtakiwa hakuruhusiwa kusema chochote kwa sababu shtaka lake Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu haina mamlaka ya kuisikiliza kesi hiyo hadi Mahakama Kuu.
Tags