Mgodi wa Dhahabu Geita GGM Wadaiwa Ushuru Zaidi ya Shilingi Bilioni 20


Halmashauri ya Mji wa Geita inaudai Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) shilingi bilioni 24.6 za Ushuru wa Huduma ambazo mgodi huo ulitakiwa kuzilipa katika miaka tisa kutoka mwaka 2004 hadi 2014.

Hata hivyo, GGM imepinga madai hayo ikisema kuwa Sheria ya Kodi ya Huduma ilitungwa mwaka 2004 na kuanza kutumika mwaka 2005.

Muwakilishi wa uongozi wa mgodi huo amesema kuwa walitakiwa kulipa dola za Marekani 200,000 na baadaye mwaka 2014 Sheria ilibadilishwa na kutakiwa kuanza kulipia asilimia 0.3 ya mapato yao ya mwaka hivyo kudai kuwa siyo sahihi kudaiwa kiasi hicho cha fedha. Tayari Halmashauri hiyo ya Mji wa Geita imekwishawasilisha hati ya madai kwa uongozi wa mgodi huo na kutoa siku 30 kulipwa dola za Marekani milioni 11.04 (shilingi bilioni 24.6) zikiwa ni malipo ya tozo ya Ushuru wa Huduma.

Suala hilo hilo liliibuliwa na Madiwani katika kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Mji wa Geita baada ya muwakilishi wa GGM, Joseph Mangilima kuomba ufafanuzi kwa Kamati ya Kudumu ya Fedha na Uongozi juu ya deni hilo.

Mwanasheria wa Halmashauri hiyo, Queen Luvanda alisema deni hilo lilitokana na taarifa iliyotolewa na Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) baada ya kufanya ukaguzi katika mgodi huo mwaka 2016.

Alisema kuwa ukaguzi huo ulianisha deni hilo ambalo inadaiwa mgodi huo uligoma kulilipa kwa kigezo kuwa Halmashauri haikuwa na Sheria Ndogo ya kudai kodi hiyo.

Tags

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ni millioni kumi tu ya Marekani. Kidogo sana. Hata hivi haiendani na thamani ya dhahabu haya majitu wanayochukua bure hapa kwenye shamba la bibi kupitia uongozi wa CCM ambao nawashangaa Watanzania wanavyozidi kuunga mkono kwa makelele, vinanda na vinubi. Hivi Watanzania mnaoungamkono uongozi wa CCM kwa miaka yote hii, angalieni mashimo makubwa wazi tunayobaki nayo. Angalieni marillioni ya pesa yakiibiwa kupitia hii mikata mibovu, ni matrillioni. Ukilinganisha na jinsi misaada tunayoipokea ni ukandamizaji mkubwa . Misaada itaua utajiri wa taifa letu. Maraisi na mawaziri wanatoa madini bure, wanakaa miaka kumi hata kudai chao kidogo shida, wanarudi kwenda kwa hawa hawa wezi wakubwa wanaotuita sisi nchi maskini kuomba vimillioni mia moja. misaada, Hivi lini Watanzania mtakuwa mashujaa kuona ukweli na mkawaambia watawala hawa wafungwe au wawalipe watanzania mali zao, bado mnawatetea. Wakati huo huo mnalia na hali bgumu ya uchumi, hamna chakula na Watawala hawawhawa wakisema hawatatoa chakula cha bure, lakini mmewashuhudia wakitoa nje mabilioni ya dhahabu, almasi, uranium bure.Ni lini mtaamka na kudai haki zenu. Lini?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hapa sio chama!! haya ni maslahi mapana ya taifa. ni watendaji tulio waamni ambao hawakuwa waaminifu na kukosa Uzalendo. walitaka na wamefaanikiwa kujinufaisha.. LAKINI AMINI KWAMBA HIVI SASA yote yako mezani kwa Jpkm na anashughulilia hili suala mpaka kieleweke.. kuwa na subira. kheri iko njiani. Magu kiboko yao...hapa kazi tu

      Delete
    2. Anonymous 9 August 2017 at 00:17
      Una comment kama uko kwenye kampeni za uchaguzi. Hivi kwa akili ya kawaida unadhani uwepo wa chama mbadala wa CCM ndio solution?
      Je, ni chama kipi hicho unachodhani kitaleta mabadiliko hayo?- Chadema? CUF? You must be kidding!

      Delete
  2. Awatumbue bsdi waliossini wote. Wengine ni max maraisi.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad