Kuna watanzania wengine wana akina za ki-zwazwa sana. Kila siku wanalalamika, ooh mara Rais hivi...ooh mara kafanya vile. Mnataka afanyeje? Afanye kama kila mtu anavyotaka amekuwa malaika?Ukiulizwa wewe umefanya nini utajibuje?
Tanzania ilishakuwa ya watu wachache walewale wanaojuana, watu maarufu.
1. Watu walikuwa wamehodhi maeneo makubwa nchi nzima, wakati hawayafanyii kazi
2. Wafanyabiashara wengi walikuwa hawalipi kodi
3. Wafanyakazi hewa, dawa hewa, mishahara hewa, pembejeo hewa,vyeo hewa
4. Wakubwa walikuwaga wanajitanua sana, walikuwa wanatunyanyasa sana. Utafikiri sisi ni wakimbizi
5. Mamikutano ya hadhara yalikuwaga kila siku makelele, wanakusanya watu ambao wanatakiwa wafanye kazi
6. Viongozi wa Serikali walikuwaga wanajilipa double payments, wanasafiri nje ya nchi kutanua tu makundi kwa makundi
7. Vimemo tu ndo vilikuwa mpango mzima. Undugu tu kila kona
8. Mafuta hewa, posho hewa, safari hewa, maiti hewa, kodi hewa
Ingekuwa ni wewe,
1. Vijana wote walioko mtaani wangekuwa wameajiliwa?
2. Watumishi wangekuwa wamepandishwa madaraja, mishahara na kupata uhamisho?
3. Ungekuwa umeondoa foleni jijini Dsm?
4. Ungeruhusu kila mtu aishi anavyotaka?
5. Ungekubali mtu akukashifu mtaani bila sababu yoyote?
Tusipotoshe umma.Tulishafikia mahala ambapo ili kuleta maisha bora, ni lazima baadhi ya watu waumie. Ilikuwa ni lazima jasho litoke.
Mtu ameingia madarakani mnataka shida zote ziondoke, ngumu ndugu zangu.
Yaani ilikuwaga taabu tupu.
Maisha mazuri yanakuja na ndo maana tunaona Mh Rais kama anatukomesha, hatupendi. Siyo hivyo.Mh Rais yupo pamoja nasi. Hiki ni kipindi cha transition tu, mambo mazuri yanakuja na kuja kwake ndo hizi harakati zinazoendelea.
Baba mwenye nyumba lazima uwe "fit" kuijenga nyumba yako. Maandalizi ni lazima yafanyike, watu wakaze mikanda. Maisha ya asali na maziwa yanakuja ,very soon tutasahau yote haya.
Tuchape kazi, Mh Rais ni mtanzania mwenzetu. Mambo mazuri yanakuja.Ana nia nzuri na sisi na ndo maana mnamuona hana mbwembwe ,yupo tu hapa nchini .Hatoki mtu hapa.
By Hivi Punde/JF
Hilo nalo neno.
ReplyDeleteIlikuwa kawaida kumchukuwa super star wa bongo ukamuhonga gari ya milioni 100 na kumkodia nyumba ya milioni2 kwa mwezi!
ReplyDeleteilikuwa kawaida kwa mfanyakazi wa TRA kuwa na nymba zaidi ya 20
ilikuwa kawaida mfanyakazi wa ikulu kumiliki ghorofa
ilikuwa kawaida mizigo kupita bandarini mamilioni ya pesa zikenda kwa wajanja kidogo.
ilikuwa kawaida Polisi wala rushwa kumcomekea mwananchi wa kawaida kesi isiyokuwa yake huku wengine wakipokea mamilioni ya pesa za wauza dawa za kulevya.
ilikuwa kawaida Viongozi wa serekali kujifanya wao ni miungu watu.
Pongezi kwa Raisi wetu MH John Pombe magufulI na sisi kina yakhe tupo nyuma yako ila kule Zanzibar kaweke mambo sawa tupe ushindi wetu wa Oct-2015. hapo utakuwa kiongozi wa kupigiwa mfano Afrika.
Ndugu yenu Hapa kazi Tu.
MAGUFULI OYEEEEEEEEEEE ANAYE SEMA ZIII MCHAWI NA ADUI NAMBA MOJA WA MAENDELEO YA WATIZI..MUNGU MBARIKI MAGUFULI,MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WAZALENDO WOTE KWA UJUMLA NA ANGAMIZA WALE WOOOOTE WASIO WAZALENDO ...AMIN.
ReplyDelete