Mimi Nipo Sexy Sana na Nina Mvuto Sidanganyiki na Vichips Mayai – Lulu Diva

Msanii wa Bongo Flava, Lulu Diva amejimwagia sifa jinsi anavyoamini kuwa yeye ni mzuri.

Muimbaji huyo amekiambia kipindi cha Uhondo cha E Fm kuwa alitambua kuwa yeye ni mzuri kutokana na sifa alizokuwa akipewa na mama yake mzazi kitu ambacho  kilimfanya kutolaghaika na watu waliokuwa wakimsifia.

“Mimi ni msichana ambaye nipo sex ambaye nina mvuto, mama yangu alikuwa akiniambia Lulu mwanangu mashallah, yaani hapa sidhani kama kuna mtu nitamwambia idadi ya ng’ombe ninazozitaka halafu akapindua,” amesema na kuongeza.

“Na mimi mwenyewe nikawa najiona ndio maana hata sikuweza kurubunika, yaani ile mtu kuniambia wewe mzuri akanidanganya kwa vichipsi mayai, mwenyewe nilishajijua ni mzuri,” amesema Lulu Diva.

Hitmaker huyo wa Usimwache kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake inayokwenda kwa jina la Utamu.

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. LULU DIVA. MIMI MBONA SIKUELEWI...!!! SASA BIASHARA IMEKUWA MITANDAONI. AU UMEKOSA SOKA..!!!?
    KWANI NANI KASEMA WEWE MBAYA?
    AU NDIYO VILE... MANAKE MAJI YAKIGUSA NYAYA LIVE NI HATARI. TULIA DADA.
    ILE POSA ULISHAJIBU..!!! SEMA NI NG'OMBE KICHAA MMOJA NA NDAMA MOJA JUMLA ZINAKUWA TATU. UKIJUMLISHA PAMOJA NA KALE KAKUKU KAMA RODA ANAKAUZA PIA. TUNANGOJA MAJIBU.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad