Mjamzito Ajifunzua Mtoto Akiwa Kwenye Kituo Cha Kupiga Kura Kenya....

Mwanamke mmoja amejifungua kwenye kituo cha kupigia kura katika mji wa Pokot Kaskazini leo muda mfupi baada ya kufika kwenye kituo tayari kwa kupiga kura yake.

Mwanamke huyo, Paulina Chemanang mkazi wa Alapat, alikwenda kwenye kituo cha kupigia kura cha Shule ya Sekondari ya Konyao Mchanganyiko na ndipo alipoanza kupatwa na uchungu wa uzazi.

“Nimefurahi sana kwakuwa hii ni baraka kwangu,” amesema na kuongeza kuwa, “kujifungua kwenye kituo cha kupigia kura ni baraka kwangu na ninamshukuru Mungu kwa hili.”

Mtoto huyo wa kike aliyezaliwa leo amepewa jina la Chepkura, kwa sababu amezaliwa wakati wa uchaguzi (kupiga kura). Hii ni kwakuwa watu wa Pokot hutoa majina kwa watoto wao kulingana na matukio makubwa yanayotokea au misimu mbalimbali.

“Sikupata maumivu ya uchungu nilipokuwa natoka nyumbani, na nilipata maumivu muda mfupi tu baada ya kufika hapa. Sikuwa na maumivu wala dalili yoyote ya kujifungua tangu jana,” alisema Paulina.

Paulina alipata msaada wa haraka wa kujifungua hapohapo kwenye kituo cha kura kutoka kwa wanawake wengine waliokuwa hapo kabla ya kupelekwa kwenye kituo cha afya akiwa na mwanaye kisha kurudishwa kituoni hapo baada ya muda ili aweze kupiga kura na kushiriki kikamilifu zoezi hilo la kuchagua viongozi anaowataka.

“Sasa nina furaha kwa sababu nimejifungua na pia nimepiga kura tayari,” alimalizia Paulina.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad