Mnaomshambulia Tundu Lissu Mkapimwe Akili...Vitendo vya Kishenzi Anavyovipinga Vinatia Taifa Letu Doa

Mnaomshambulia Tundu Lissu Mkapimwe Akili...Vitendo vya Kishenzi Anavyovipinga Vinatia Taifa Letu Doa

Ndugu zangu amani iwe nanyi, nasema kwa uwazi mnaomshambulia na kumkejeli Tundu Lissu hamjitambui inawapasa mujitathimini.

Nasema haya kwa sababu tamko la kutaka mawakili wagome halijatolewa na lisu limetolewa na baraza la uongozi TLS.

Pia nawaasa msilijukulie swala hili kisiasa kwani sio la kisiasa,.nilitegemea watanzania kwa umoja wetu tulaani tukio hilo la kigaidi la kuteka walinzi na kulipua ofisi za mawakili.

Naomba niwakumbushe historia japo kidogo, kwa miaka yote tangu uhuru TLS imekuwa ikiongozwa na makada wa CCM na kiukweli ilipoteza mwelekeo na kuwa tawi la CCM.

Katika kipindi chote hicho ili uwe rais wa TLS ilikuwa lazima uwe kada wa CCM. Hata katika uchaguzi uliomweka Lissu kuwa mwenyekiti wa TLS uligubikwa na nizengwe mingi ikiwemo kuingiliwa na serikali.

 Niwakumbushe pia katika uchaguzi wa TLS tulishuhudia kila mizengwe ya kumkwamisha Lisu asogombee Urais ikiwemo kukamatwa airport na kuwekwa ndani mpaka mahakama ilipoamuru apewe dhamani cku ili ili ya uchaguzi.

Nawashauri ndugu zangu tuache siasa za kijinga kwenye masuala yanayogusa maisha ya binadamu, maana wale walinzi wanafamilia zao wangeweza hata kuuwawa nani anajali?

Tumeshuhudia watu wakipotezwa, maiti zikiokotwa kwenye viroba zikielea mtoni, leo ofisi za mawakili zinalipuliwa nani anajua kesho kutatokea nn au zamu ya nani?

Tuache ushabiki wa kisiasa kwa pamoja tulaani vitendo hivi vya kishenzi vinavyolitia doa taifa letu Tanzania mbele ya uso wa dunia.

Mungu ibariki Afrika.
Imeandikwa na Kimpawwe/JF

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. TUNDU LISU ,SIASA ZA KALE ,UNATAFUTA KIKI
    HATA KAMA ANATAKA UMAARUFU THIS IS TOO MUCH.PUNGUZA SIFA ZA KIJINGA ,BINAFSI NIMESHACHOKA KUKUANGALIA HATA KWENYE TV.

    ReplyDelete
  2. Kwani ungetoa maoni yako pasi na kuwaita watu wajinga ujumbe usingewafikia? Tumia nguvu ya hoja usomeke. Na ujue kila mtu ana mtazamo wake kutokana na uelewa wake, tafakari.

    ReplyDelete
  3. Lisu ..si mgeni kwetu. Tunamfahamu vilivyo ni kijana wa zamani.
    lisu ni Analog na amejisahau kwamba sisi tumesha cheji kudigitali. kwa hiyo anataka kujaribu hahati yake dhidi ya matakwa ya walimuweka kwamba anaweza kuhamasisha umma kiuchochezi ili aweze kufikia popularity ambayo hata akiamua siku za mbele kuanziaha Act mama ataweza kupata wafuasi wa Act watoto
    sasa asilo lijua ni kwamba WATANZANIA wameshaamsoma Nia yake mbaya na njia anayo tumia kufikia Malengo Tarajiwa Ote ni njia chafu na kama sikosei mtowe ameshaanza kumuelewa vizuri na uhusiano unaanza kufifia.
    uxhochezi wake uko katika njia tofauti na mbinu tofauti lakini zote ni za kitoto na inabidi aje kuripoti hii leo na inaweza tuka kaanae muda zaidi kutokana na haya.
    Na tulivyo sikia ni kwamba Afya yake inaanza kuporomoka au kuwa si ya kawaida. Lakini hayo yote tutayajua.
    Rundu bovu kaa chonjo saa mbaya kijana.

    ReplyDelete
  4. Lisu ..si mgeni kwetu. Tunamfahamu vilivyo ni kijana wa zamani.
    lisu ni Analog na amejisahau kwamba sisi tumesha changei into Digitali. kwa hiyo anataka kujaribu hahati yake dhidi ya matakwa ya walimuweka kwamba anaweza kuhamasisha umma kiuchochezi ili aweze kufikia popularity ambayo hata akiamua siku za mbele kuanziaha CDM mama ataweza kupata wafuasi wa CDM toto
    sasa asilo lijua ni kwamba WATANZANIA wameshaamsoma Nia yake mbaya na njia anayo tumia kufikia Malengo Tarajiwa Zote ni njia chafu na kama sikosei mtowe ameshaanza kumuelewa vizuri na uhusiano unaanza kufifia.
    uchochezi wake uko katika njia tofauti na mbinu tofauti lakini zote ni za kitoto na inabidi aje kuripoti hii leo na inaweza tuka kaanae muda zaidi kutokana na haya.
    Na tulivyo sikia ni kwamba Afya yake inaanza kuporomoka au kuwa si ya kawaida. Lakini hayo yote tutayajua.

    Wakati wa Lelemama umeshapita.
    HII NI TANZANIA YA KUFANYA KAZI NA KUJITUMA ILI UISHIKAMA ULIZOEA KUUZA MANENO UTAUZA SANA. NA SOKO LIMEDORORA .. ITABIDI UNUNUE MWENYEWE..PATAMU HAPO.

    ReplyDelete
  5. Kazi bila sheria chini ya uamuzi wa mtu mmoja hivi nyinyi mnazo kichwani au. Papara za uongozi maima wa CCM bila kutuliza na kufikiri, bo,oa, eti hawatoa vibali, wako Dar au hawapo. Amri ya mtu mmoja iongoze nchi. Hivi nyinyi mna akili au. Raisi, Makonda wanasema hawajui bomoa bomoa, nani Mtanzania mjinga, ipo kwenye TV kila siku, simu watu wamepigiwa . Hii inaonyesha wazi watawala hawapo na wananchi. Wanakaa nchi mbili tofauti. Ndo maana tunajiuliza Lini CCM na utawala wa CCM na Watanzania wanaoitetea, kupiga mabomu ni jinai kubwa. Hawachukulii serious pamoja nanyi mnao,kosoa Lisu. Mnaijua Amani tuliyokuwa nayo ambayo inapotea. Polisi tunao na mnawalipa kodi. Usalama tunao ingebidi wajibu na hata Raisi wa nchi angekuwa mtu wa kwanza kukemea ili kuwatuliza na kuwapa emani wananchi. Sijamsikia. Kila nchi inapotupiwa bomu, kunwa au dogo, Kiongozi wa nchi lazima asimame akemee na awahakikishia wananchi kwamba haitatokea tena kamwe kwa Mtanzania yeyote, Nawashangaa watu, wananchi mnamlaumu mtu anayelichukulia hili swala seriously. Niwaulize nyinyi ni Watanzania wapenda amani au. Mnapolikubali kila jambo serikali linafanya hata makosa mnalipigia makofi. Sasa tunamtafuta mchawi ili tuendelee tukiona wengi wetu hawana maarifa, hawajui kufikiri, hawapo aggessive kuwa huru, kuwa na amani ,kupatiwa chansi ya kujiendeleza na kupewa usawa kwenye ajira, badala yake ni kutoa utumbo mmoja baada ya mwingine huu ni umaskini wa kufikiri ulioukithiri nchi hii kwa miaka. Hata tukiamshwa bado tunalala fofofo. Hivi tunaujinga mkubwa wa namna hii basi hakuna hope ya uhuru wa kweli, wala maendeleo ya kweli licha ya kubabaisha na Wawekezaji wanaotutumia wakijua Taifa na watu bado wamelala baada ya miaka hamsini.
    NI AIBU KUBWA SANA. Na nyinyi hapo juu hamjui ninalolizungumza limewazidi ujuzi na uelewa wenu.Mjiombee.Ndo maana tuna makanisa kila kona tusiamke na kujitambua tukijazana makanisani kulia na kuomboleza badala ya kujisomesha tufunguke.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad