Mwenyekiti wa Bodi ya Msamaha kwa Wafungwa (Parole), Augustine Mrema ametoa shukrani zake kwa Rais John Magufuli kwa kumsaidia kupata matibabu nchini India na kufanikiwa kupona ugonjwa wa kansa.
Mrema alisema kwa sasa utendaji wake wa kazi utaimarika kwa kuwa ameshapona ugonjwa uliokuwa ukimsumbua na kushindwa kutumikia wananchi na Taifa.
Akizungumza mbele ya waumini wa Kanisa Katoliki Parokia ya Bikira Maria Mama Mwokozi jijini Dar es Salaam, alisema kuanzia sasa atamsaidia vizuri Rais katika nafasi yake ya kuwatetea wafungwa kupitia msamaha wa Bodi ya Parole.
Alisema amefikia hatua ya kutoa shukrani kwa sababu ya muujiza aliopata kutoka kwa viongozi wa Serikali na dini waliomuombea.
Paroko Kiongozi wa kanisa hilo, Cathbert Magaga aliwataka waumini wengine kuiga mfano wa Mrema wa kutoa shukrani na siyo kunyamaza kwa kuwa Mungu atawasaidia.
Ni vizuri Umesaidiwa na Magufuli. Tatizo ni mfumo wa chama, mfumo wa serikali na mfumo wa sera. Kwa nini Magufuli tu ndo asifike kufanya vitu binafsi kusaidia mtu kama wewe na ukaridhia. Je wangapi wanakufa vijijini ambao hawapo karibu na Magufuli? Vitu kama hivi ambavyo vinawafanya viongozi kama wewe kukubali kisa umesaidiwa na Raisi Vinawapumbaza Watanzania. Bafala ya kupigania mfumo mzima wa serikali unamsaidia au umsaidie kila Mtanzania bila kujuana au kupitia kwa raisi. Sasa unataka wote tuwe karibu na raisi ndipo tupate huduma, badala ya kupeleka vigezo vyote nchi nzima ili watu wawe na huduma nzuri kila mtaa, wilaya, mkoa? mnauza nchi kwa kuchangia vijisehemu vya maendeleo au huduma kwa wachache walio na vyeo na ukaribu wa raisi badala ya kupigania mkate mzima kwamba hii ni haki ya kila Mtanzania awe tajiri au maskini, awe mjini au vijijini, awe CCM au chadema . Badala yake mnakuwa short sided na kuridhia upendeleo na ubaguzi kama huu. Najua wengi wapo gizani kuona hili. Kila kiongozi awe CCM au Chadema asaidiwe na serikali sawa katika kutatua matatizo ya Wananchi popote walipo. Lakini wengi mnashindwa kuuona upendeleo kichama, kikundi, na kikabila. Kuna kuchagua hapa na pale na huu ni upendeleo. Mpaka tutakapoona maskini wanathaminiwa kama viongozi hao wanavyosema . Lakini hawafanyi hivi. Kuna watoto wa maskini wanakufa wanapewa dischaji sababu hawana fees ndogo sana. Wanatolewa Mhimbili kila siku,. Kisa. ni mwanamke peke yake, hana kipato anauza kila kitu wakati mwingine anachoshindwa ni usafiri wa basi na chakula. Watoto wao wanawafia mikononi mwao kila siku. Nyinyi vigogo mnakwenda India, mnasaidiana na kuhakikisha mnapata huduma safi, sababu mnajuana. Hii ipo kila siku tunaiona. Maneno yenu hayaendani na vitendo vyenu. Acheni kiuza Nchi sababu eti umesaidiwa na raisi badala ya kuhakikisha huduma uliyopewa ni haki ya kila Mtanzania.Hii inauma na akili fupi, na uvivu wa kuifikiria nchi na unajifikiria mwenyewe tu. Lini viongozi mtaona mbali mdai usawa kwa kila mtu.Inasikitisha, inaaibisha, na inashangaza. Acheni hizi gereshageresha mkijua wengi Watanzania upeo wao wa kuona mbali ni mdogo. Ndo maana mmechaguliwa, au kuteuliwa kuleta mabadiliko ya kweli.
ReplyDelete