Msemaji wa Serikali Akiri Ndege Mpya ya Bombardier Q 400-Dash 8 Kushikiliwa Nchini Canada. Awatupia Lawama Wanasiasa...


Ununuzi wa ndege ya 3 ya Bombadier umeingiliwa na mgogoro uliotengenezwa na wanasiasa na watu wasioitakia mema Tanzania.

"Wanasiasa waliotengeneza mgogoro huo wanahujumu maendeleo ya nchi na usalama wa raia"-Kaimu Mkurugenzi Mkuu-Idara ya Habari Zamaradi Kawawa

Ndege ya 3 ya Bombadier ipo na inakuja kwahiyo wananchi waiamini Serikali yao. Serikali imesikitishwa na ushiriki wa wanasiasa na baadhi ya watu kuhujumu maendeleo ya nchi.

Watanzania tuwe wazalendo kulinda,kutetea na kukabiliana na hujuma zozote zinazorudisha nyuma maendeleo ya Nchi.

Watanzania, Tuunge mkono jitihada za Rais Magufuli katika kuleta maendeleo bila kujali itikadi ya chama, kabila au dini. Kuhusiana na mgogoro wa ununuzi wa ndege hatua za Kidiplomasia na sheria zimeanza kuchukuliwa ili kumaliza jambo hili.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hao au hilo kundi ni watu hatariiii kwa mustalanali wa Taifa. Hilo ni kundi tu la watu ambao wanadhani kwamba wanaweza kuliendesha Taifa kwa manufaa yao na wanavyoraka wao na nafsi zao na familia zao. Maisha yao yawe juu. Na wenzao yawe chini.Ili waendelee kuwaburuza wenzao na maisha ya kifukara na umasikini

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad