MSIGWA: Pole Pole Hana Uwezo wa Kumuondoa Kwenye Jimbo la Iringa

MSIGWA: Pole Pole Hana Uwezo wa Kumuondoa Kwenye Jimbo la Iringa
Mbunge wa Iringa Mjini kwa tiketi ya (CHADEMA), Mchungaji Peter Msigwa ameibuka na kumjibu Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole na kumwambia kuwa hana uwezo wa kumuondoa kwenye jimbo la Iringa Mjini 2020 kama alivyoahidi.

Mchungaji Msingwa amesema hayo kupitia ukurasa wake wa Twitter na kumtaka Humphrey PolePole kuwauliza wenzake ambao walimtangulia katika nafasi yake hiyo ya Uenezi kuwa watampa majibu.

"PolePole huna uwezo huo waulize wenzio waliokutangulia , mimi sijateuliwa kama wewe" alisema Mchungaji Msingwa

Siku mbili zilizopita Mchungaji Msigwa alisema kitendo cha Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Msukuma kusema anamkumbuka Mbunge wa Mtama Mhe. Nape Nnauye ni ishara kuwa Humphery PolePole ameshindwa kuvaa vizuri kiatu alichoachiwa kama Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, ndipo hapo PolePole alipokuja na kumwambia Msigwa kuwa huu ni wakati wake wa mwisho kama Mbunge wa Iringa Mjini.

"Kitu kimoja nakuahidi, hii ni 'term' yako ya mwisho, tunakurudisha kufanya kazi ya Uchungaji maana naona Mchungaji anajichanganya na mbuzi" alisema Humphery PolePole
Hata hivyo siku moja baada ya ahadi ya Humphery PolePole madiwani watatu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Iringa Mjini walitangaza kujiuzulu nafasi zao kwa kile walichodai kuwa viongozi wa juu wa chama hicho Iringa wamekuwa wakiwatenga na kuwatuhumu kuwa ni wasaliti, hivyo wameamua kujiuzulu nafasi zao kama madiwani.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad