Mtatiro Yamemfika Hapa...Adai ni Bora Kufanya Kazi na CCM Kuliko Lipumba

Mtatiro Yamemfika Hapa...Adai ni Bora Kufanya Kazi na CCM Kuliko Lipumba
Mwenyekiti Kamati ya muda ya uongozi wa CUF, Julius Mtatiro amefunguka na kujibu hoja za baadhi ya watu ambao wanataka CUF kukubaliana na Professa Lipumba kwa kuwa Mwenyekiti huyo ameshika makali kutokana na vyombo mbalimbali vya serikali kumtambua.

Julius Mtatiro ambaye sasa yupo nchini Marekani alipokwenda kimasomo amesema hilo kupitia mtandao wake wa Facebook na kusema ni jambo ambalo halitawezekana wao kukubali yaishe na Profesa Lipumba na kusema wataendelea na harakati zao kuhakikisha haki yao inapatikana.

"Nasoma maoni ya baadhi ya watanzania kuja kwetu, kwamba kwa sababu serikali, dola, CCM, polisi, bunge, NEC, RITA, na Msajili wa Vyama vya Siasa wameshikamana kumuunga mkono Lipumba, na kwa hiyo ati Lipumba ameshikilia mpini na chama kimeshikilia makali kwa nini tusikubali yaishe? Lipumba apewe kila kitu...hadi roho zetu, lakini misingi yetu, misimamo yetu, umoja wetu na mshikamano wetu, hawezi kupewa. Hizi ndizo silaha zetu na niwaambie kuwa zina faida ya muda mrefu kuliko zile anazozitizama msaliti" alisema Mtatiro
Aidha Mtatiro anasema kuwa ni rahisi sana wao kufanya kazi na CCM kuliko kufanya kazi na Profesa Lipumba

"Ni mara kumi kumsamehe jirani yako aliyembaka mwanao, kuliko kumsamehe baba yako mzazi aliyembaka mwanao. Adui wa ndani, ni hatari zaidi kuliko adui wa nje. CCM ni adui bora kuliko Lipumba na kwa hiyo ni rahisi sana kufanya kazi na CCM kuliko kufanya kazi na Lipumba" alisisitiza Mtatiro

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Unataka kuniambia misingi yenu inaendana na ccm. Je unaujua na kuukubali uhuru wa fikra. kama kunajambo unalipigania na wewe ni mtanzania hasa, ndio utafanya kazi na ccm sababu ni kimeshika dola kwa sasa, lakini nitashangaa baada ya masomo yako kuja na kujiunga na CCM unajua wazi ccm kina msimamo gani. Angalia wapi kumetupeleka mpaka hapa tulipo. ni Mfumo mzima umenuka. Sidhani kama kuna mkono safi ndani ya chama hiki kwa sasa tukitafuta ukweli. Ingawa tunaambiwa visivyo kwa sasa, lakini sikiamini kutendea haki Watanzania sababu wengi waliohusika bado hawajatumbuliwa na bado wanaongoza nyuma ya pazia.

    ReplyDelete
    Replies
    1. hujielewi na wala hujitambui unayenuka ni wewe ambaye huna shukrani hata kwa kidogo

      Delete

Top Post Ad

Below Post Ad