Mwaka 2016 Mbaya kwa Habari Zinazochapishwa Kutokana na kuwepo Kwa Sheria Kandamizi
0
August 14, 2017
Uwepo wa sheria kandamizi zinazoratibu magazeti umechangia kwa kiasi kikubwa mwaka 2016 kuwa mbaya kwa habari zinazochapishwa.
Hilo limeanishwa kwenye ripoti ya hali ya vyombo vya habari mwaka 2016 katika utafiti uliofanywa na Baraza la Habari Tanzania (MCT).
Akiwasilisha ripoti hiyo leo Jumatatu, Dk Joyce Bazira amesema licha ya magazeti kujikongoja hali ilikuwa mbaya.
Amesema yapo magazeti na majarida ambayo yaliamua kujiondoa yenyewe sokoni kutokana na uwepo wa sheria hizo.
Amesema kwa mwaka jana pekee jumla magazeti 437 yalifutwa kwa pamoja.
"Haijawahi kutokea magazeti mengi hivi yakafungwa kwa pamoja ndiyo sababu tumeona ilikuwa mwaka mbaya kwa magazeti."
Amesema kulikuwepo pia suala la kushuka kwa matangazo na usambazaji wa magazeti unapungua.
"Tunaona mwaka 2016 usambazaji na mauzo ya magazeti yalipungua mno na hii ni kutokana na uwepo wa mitandao ya kijamii,"
Amesema takwimu zinaonyesha mwaka 2016 magazeti machache yamesajiliwa ikilinganishwa na mwaka 2015.
Tags