Mwanasheria Tundu Lissu Apinga Ushahidi Uliotelewa Dhidi ya Wema Sepetu

Wakili Tundu Lissu ameukataa ushahidi unaoendelea kutolewa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam dhidi ya msanii  Wema Sepetu kwa madai wakili wa serikali aliiambia mahakama kuwa ushahidi huo ulikuwepo lakini  haukuwa ndani ya bahasha.

Ushahidi huo uliowasilishwa kutoka Ofisi ya Mkemia Mkuu wa serikali ulipingwa na mawakili wanaomtetea Wema Sepetu akiwemo Tundu Lissu pamoja na Peter Kibatala
Ofisa kutoka Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali alipeleka vithibitisho anavyotuhumiwa kukutwa navyo Wema Sepetu na watuhumiwa wengine wawili ambavyo ni misokoto miwili ya bangi ambayo ilikuwa imefungwa katika bahasha.

Katika hoja ya wakili wa serikali kwamba bahasha ndiyo ushahidi aliiondoa baada ya kutakiwa kueleza kilichokuwemo ndani ya bahasha ili kitambulike kama ushahidi.

Baada ya kuondoa hoja hiyo, Hakimu wa Mahakama hiyo Thomas Simba alimwamuru mtoa ushahidi kuifungua bahasha, japo upande wa utetezi uliukataa ushahidi huo kwa madai kuwa ndani ya bahasha hiyo kulikuwa na vielelezo vingine ambavyo mtoa ushahidi hakuvieleza awali, kikiwemo kitu kilichodhaniwa kuwa ni karatasi nyekundu.

Baada ya kusikiliza hoja hizo hakimu aliiahirisha kesi hiyo hadi Agosti 18 ili aweze kutoa ufafanuzi juu ya ushahidi huo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad