MZEE MAJUTO:Hali Yangu Haijatengemaa Bado Naumwa


MZEE MAJUTO:Hali Yangu Haijatengemaa Bado Naumwa
Mungu tenda! Ikiwa ni siku chache tangu muigizaji mkongwe, Amri Athman Amri ‘King Majuto’ kupata unafuu kufuatia upasuaji aliofanyiwa kutokana na tatizo la ugonjwa wa ngiri (hernia), hali yake bado haijatengemaa na anatumia muda mwingi kulala, Amani limezungumza naye kwa tabutabu.

Jumatatu ya wiki hii, mwandishi wetu alimpigia simu mzee huyo kwa lengo la kumjulia hali na kufanya naye mazungumzo mengine, lakini King Majuto alisikika kwa shida na kudai amelala na anahitaji muda mwingi wa kupumzika na kwamba bado anaumwa na anasikia maumivu makali.

Hata hivyo, mwandishi aliendelea kumdadisi kwa kina ili kujua ni nini hasa kinachoendelea kumsumbua kwani kama ni tatizo la awali alishafanyiwa upasuaji, ambapo aligoma kabisa kuendelea na mazungumzo na kugeuka ‘mbogo’ kwa muda kwa madai ya kutopenda mazungumzo na wanahabari.

“Bado nimelala jamani na sijui unataka nini tena? Naumwa na ninasikia maumivu sana na sitaki kuzungumza zaidi maana nimechoka, elewa tu kwamba bado naumwa na ningependa sana uniache ili nipate muda mwingi wa kupumzika, ni kweli hivi karibuni nilipata nafuu kabisa na kuanza kutembea lakini ndiyo hivyo bwana, bado hali haijakaa sawa,” alisema King Majuto.

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mungu atakuafu akupe Afya Inshaallah. Kwa baraka za zihi kumi zA Dhull hija

    ReplyDelete
  2. KING..Mungu atakuafu akupe Afya Inshaallah. Kwa baraka za HIzi kumi za Dhull hija na utakula Eid Al Adha kwa afya na furaha

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad