Neymar Afunguka Baada ya kucheza Mechi Yake ya Kwanza Paris St-Germain



 Neymar Afunguka Baada ya kucheza  Mechi Yake ya Kwanza Paris St-Germain
Neymar alifunga bao mechi yake ya kwanza katika klabu yake mpya ya Paris St-Germain baada ya kununuliwa kwa rekodi ya dunia ya £200m kutokaBarcelona.

Raia huyo wa Brazil alichangia katika mabao yote matatu yaliyofungwa na PSG dhidi ya Guingamp ambao wamefanikiwa kudumisha rekodi yao ya kushinda 100% mwanzo wa msimu.
Jordan Ikoko alifungua ukurasa wa mabao kwa kujifunga baada ya pasi ya Neymar kwa Edinson Cavani kuzimwa

Neymar kisha alimsaidia Cavani kufunga kwa pasi safi kabla ya nyota huyo wa uruguay naye kumpa pasi Neymar ambaye alifunga dakika za mwishomwisho akiwa hatua sita hivi kutoka kwenye lango.
PSG wamnunua Neymar kwa rekodi ya dunia ya £200m
Mchezaji huyo wa Brazil mwenye miaka 25 alichezeshwa upande wa kushoto lakini alihusika kati safu ya mashambulizi.

Alitamba sana uwanjani kwa kugeresha na kushambulia, ingawa mengi ya makombora yake yalizimwa kabla yake kufanikiwa kufunga dakika za mwisho.

Neymar aligusa mpira mara 128 - mara pili kwa wingi mechi ya ligi Ulaya
Akilinganishwa na washambuliaji wenzake Edinson Cavani na Angel di Maria
Makombora6, pamoja na yaliyozimwa(sawa na Cavani na Di Maria)

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad