Nionyeshe marafiki wa Mh Tundu Lissu Nami Nitakuonyesha Oligaki, Aristrokasi na Timokrasi

Nimepata nafasi ya kumsikiliza Mh Tundu Lissu alipozungumzia suala la la ndege ya bombardia ambayo serikali ya Tanzania inailipia ili iinunue kule nchini Kanada. Lakini kwanza ninaona ni vyema nieleze matabaka ambayo yanaweza kujengeka kwenye jamii kabla ya kutoa maoni yangu kuhusu suala hili.

Wataalam wa sayansi ya jamii wanasema, kutokana na unyonyaji au uporaji wa uchumi ambao unaweza kufanywa kwa njia mbalimbali za kifisadi na kikundi cha watu husababisha kujengeka kwa matabaka katika jamii. Tabaka la kwanza ni la matajiri ambalo humilki sehemu kubwa ya uchumi wa nchi kwa njia ya ufisadi au unyonyaji. Kwa lugha ya kigiriki, tabaka hili linaitwa origarchy (oligaki).

Oligaki huweka rais wao madarakani ili waweze waweze kuendelea kupora utajiri kwa kumtumia rais waliyemweka madarakani. Oligaki wataweka majaji wao kwenye mhimili wa mahakama ili wakiwa na kesi waweze kushinda. Oligaki wataweka watu wao kwenye vyombo vya usalama, wataweka wabunge na madiwani wao ili maamuzi yatakayopitishwa yaweze kuwanufaisha wao.

Kuwepo kwa tabaka hili husababisha kuwepo na matumizi makubwa ya fedha kwenye chaguzi. Oligaki hutumia fedha nyingi kuwanunua watu ili wawapitishe wagombea wao kwenye chaguzi hizo. Wagombea wanaofadhiliwa na oligaki hupita makanisani, misikitini na kwenye jamii wakitoa misaada mbali mbali ili wapate kukubalika hatimae wachaguliwe. Lakini baada ya kuchaguliwa hutetea maslahi ya oligaki badala ya maslahi ya wananchi.

Tabaka la pili ni lile la marafiki au ndugu wa oligaki. Tabaka hili huitwa aristrocracy (asistrokasi). Aristrokasi ni watu waliowekwa na origaki ambao wapo kwenye taasisi za fedha, ubalozi, serikalini, na vyama vya siasa. Tabaka hili kazi yake ni kutetea na kulinda maslahi ya mafisadi ambao hutafuta kushika au wameshika njia kuu za uchumi za nchi na hivyo tabaka hili huwa na upinzani mkubwa na serikali na kwenye bunge kwa lengo lakutetea maslahi ya matajiri. Aidha, tabaka hili hujivika ngozi ya kondoo, kwa kujiita watetezi wa watu wanyonge.

Tabaka la tatu ni la watu wenye tamaa ya madaraka, tabaka hili huitwa timocracy (timokrasi). Watu walioko kwenye tabaka hili huunga mkono hoja za oligaki na aristrokasi na hutamani siku moja waingie kwenye matabaka hayo. Timokrasi ni watu wasio na msimamo wowote, kwani wametawaliwa na tamaa na makuu na kiburi na ubinafsi. Timokrasi ni wepesi kuwasaliti wananchi. Hawana chembe ya uzalendo kwa nchi yao. Timokrasi ni wanafiki. Na mnafiki humtukuza yeyote, kwa lolote, kwa matumaini ya chochote; ndivyo walivyo.

Tabaka la nne ni la wanachi maskini wanaotegemea maisha bora kutoka kwenye serikali walioichagua.

Matabaka haya yamejengeka kwa kasi sana hapa nchini kuanzia mwishoni mwa utawala wa rais Mkapa. Kutokana na kuwepo kwa matabaka haya watanzania masikini waliendelea kushuhudia utajiri wan chi hii ukiwanufaisha watu wachache walioko kwenye matabaka ya oligaki,aristrokasi na timokrasi. Serikali ya awamu ya tano imeonyesha dhamira ya kweli ya kuhakikisha rasilimali za nchi hii zinawanufaisha watu watanzania wote. Lakini ni dhahiri pia kwamba tabaka la oligaki, aristrokasi na timokrasi hawafurahishwi na jitihada za serikali hivyo wanapambanma kuhakikisha juhudi za serikali hazifanikiwi. Ni dhahiri nchi yetu iko kwenye vita ya uchumi. Vita hii ni ngumu sana kupita vita ya kupigania uhuru. Katika vita hii ya uchumi, wapo watanzania watakaogeuka mawe na kuwa wasaliti wakiungana na oligaki lakini wakijificha kwa kuvaa ngozi ya kondoo, wakijifanya ni watetezi wa watanzania maskini wakati ni watetezi wa mafisadi(oligaki).

Hivi Karibuni nilipata nafasi ya kumsikiliza Mheshimiwa Tundu Antipas Lissu mbunge wa jimbo la Singida Mashariki alipokuwa akichangia kuhusu suala la hatua ambazo zimechukuliwa na seriklai kuhusu makinikia au mabaki ya mchanga kutoka kwenye migodi ya dhahabu. Kwa upande wangu nilimuona alitumia lugha kali sana na alikuwa na ghadhabu. Nilijiuliza sana kuhusu mchango alioutoa na ghadhabu alizoonyesha. Imebidi nijaribu kufuatilia misismamo yake, huu ni mtazamo wangu tu.

Mwaka 2015 wakati Lowassa anahamia Chadema kutoka CCM nilipata taabu kubwa nilipomwona Tundu Lissu akiwa ndiye alikuwa akimtetea Lowassa kuhamia Chadema na akimlaumu Dk Slaa.
Wakati wa kampeni 2015 UKAWA ilikuwa na kazi ngumu kuwashawishi watanzania kuhusu suala la ufisadi. Ajenda ya ufisadi ikafa. Uchaguzi ukafanyika, watanzania wakaamua waendelee kuongozwa na CCM. CCM ikaunda serikali.

Serikali ya CCM chini ya uongozi wa John Pombe Magufuli (JPM) ikaanza kushughulikia suala la ubadhirifu, uzembe, na maadili kwa watumishi wa umma. Watumishi wengi walichukuliwa hatua kali na serikali ya CCM chini ya uongozi wa JPM. Mtakumbuka, kuna kiongozi a;liyekuwa analipwa mishahara 17. Mtakumbuka uozo kwenye bandari ya Dar es salaam. Na mtakumbuka kwamba walipatikana wafanya kazi hewa zaidi ya elfu 10, wanafunzi hewa na suala la madawa ya kulevya.
Tundu Lissu na Chadema walilalamika juu ya hatua zilizochukuliwa na serikali, wakisema watu hao waliochukuliwa hatua wanaonewa au utaratibu uliotumika ni mbovu. Mashaka yangu juu ya Mheshimiwa Tundu Lissu yakazidi kuwa makubwa.

Lakini pia mtakumbuka kuhusu suala la UKUTA. Wabunge wa UKAWA walikuwa wakifunga midomo wakiwa bungeni wakidai demokrasia pana. Lakini kwa sasa ni dhahiri kwa watu wengi kuwa ndani ya CCM kuna demokrasia pana kuliko ndani ya Chadema. Hili limedhibitishwa na uchaguzi wa wabunge wa bunge la Afrika Mashariki. CCM ilifanya mchakato wa kidemokrasia kuwapata wabunge wa Afrika Mashariki kuliko ilivyokuwa ndani ya Chadema. Haya yote yaliyofanyika ndani ya Chadema Lissu akiwemo na ni mwanasheria Mkuu wa Chadema. Ninaanza kujiridhisha kwamba Mheshimiwa Tundu Lissu siye niliyemfahamu.

Rais John Pombe Magufuli amedhubutu kuchukua hatua juu ya upotevu wa mapato yaliyotokana na kupelekwa makinikia nje ya nchi na kuagiza uchunguzi ufanyike. Ripoti ya uchunguzi imefichua ufisadi wa kutisha kwenye usafirishaji wa makinikia nje ya nchi. Watanzania wengi wazalendo waliosikiliza ripoti hiyo wameumia sana kwa taarifa zilizomo kwenye ripoti hiyo. Watanzania tumenyonywa kiasi cha kutosha.

Mliopata nafasi ya kumsikiliza Mheshimiwa Tundu Antipas Lissu, amesema Rais amefanya jambo la hovyo sana. Na alionekana kukasirika sana. Hiki kimenishitua sana na ninashawishika kuamini kwamba Lissu hayuko sawa, ana ulemavu usioonekana kwa macho. Tundu Lissu ni mwanasheria mzuri sana lakini amekosa roho ya kuipenda nchi yake, amekosa chembe ya roho ya uzalendo.
Nina amini vyama vya siasa vinatakiwa kuungana katika masuala ambayo yana maslahi mapana kitaifa kama hili suala la makinikia kupelekwa nje ya nchi. Aidha, wataalamu wanatakiwa kujitokeza kutoa ushauri namna ya kuboresha ripoti iliyotolewa na kuisaidia serikali ili iweze kuisaidia serikali kuchukua hatua sitahiki. Lakini Tundu Lissu alikebehi au kudhihaki hatua ikliyochukuliwa na serikali.

Wapo watanzania wengi waliomwamini sana Tundu Lissu na wanataabika na misimamo yake ya hivi karibuni kama ninavyotaabika mimi.

Serikali ya awamu ya tano imefanya utaratibu wa kununua ndege kutoka Canada kwa lengo la kuboresha usafiri wa anga na kuinua utalii nchini. Bila shaka watanzania wengi wanaunga mkono jitihada hizi za serikali kwani ilikuwa ni aibu kwa nchi yetu ilipokuwa haina ndege hata moja.
Siku chache zilizopita, Mh Tundu Lissu ameeleza kuwa ndege aina ya bombardier mali ya serikali ya Tanzania imeshikiliwa huko Kanada na kampuni moja ya ujenzi kutokana na kuidai serikali ya Tanzania. Iwe ni kweli au siyo kweli hoja yangu siyo hiyo. Kinachoendelea kunitaabisha ni kwa nini Mh Tundu Lissu anaonekana kufurahia nchi kupata tatizo hili na matatizo mengine yaliyopita. Haonyeshi kusononeshwa nchi yake inapopata matatizo au misukosuko. Nchi inapopata matatizo au misukosuko Mh Lissu huchekelea. Mtakumbuka serikali ilipochukua hatua dhidi ya ubadhirifu kwenye halmashauri Mh Lissu alisema wafanyakazi waliotumbuliwa walionewa na alisema atawatetea mahakamani, kwenye suala la makinikia Mh Lissu alisema Rais amefanya maamuzi ya hovyo sana na serikali itashitakiwa. Juzi Mh Tundu Lissu alionekana kufurahia ndege ya bombardier kushikiliwa na Kanada. Mh Lissu ni mbunge angeweza kuishauri serikali akiwa bungeni lakini ameona ni vizuri kwake kuidhalilisha serikali kwenye vyombo vya habari.

Mh Lissu haoni kabisa nia njema ya serikali ya kununua ndege ili kuboresha usafiri wa anga nchini. Mh Lissu haoni kabisa nia njema ya serikali kuhakikisha madini yetu yanawanufaisha watanzania, mh Lissu haoni kabisa jitihada za serikali kupiga vita ubadhirifu kwa watumishi wa serikali na halmashauri zetu, Mh Tundu Lissu haoni kabisa jitihada za serikali kuboresha elimu na huduma za afya ? Ghadhabu za Mh Lissu zinatokana na nini hasa ? Au Mh Lissu ana mtetea nani katika hoja zake kama haoni jitihada za serikali zinazowalenga wanachi maskini ?

Je katika misimamo ambayo Mh Lissu ameionyesha kwenye suala la makinikia, suala la ununuzi wa ndege, anampigania au ana mtetea nani ? Nionyeshe marafiki wa Mh Tundu Lissu nami Nitakuonyesha Oligaki, Aristrokasi, na Timokrasi.

By Fred Mpendazoe
Tags

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Inavyo onekana nikama unabusara sana lakini sinauhakika ningependa kujua mabo kadhaa kutoka kwako.lakwanza tunaishukuru serwkali kwakushughulika na mafisadi lakini ningependa kujua kama Lowasa alikua fisadi kweli kwanini hashuhulikiwi. Pili kabla ya mheshimiwa sana Tundulisi kuongelea kukamatwa kwa bombadia mbona serekali ilikua kimya haikusema kama ndege imezuiwa lakini baada ya lisu ndio tumeanza kusikia wakiongea. Tatu unapozunguzia demokrasia maana yake ninini? Uhuru wavyama vya upinzani upo au haupo mambona wapinzani wakiongea kidogo unasikia kakamatwa kwa uchochezi? Kama ccm wanaamini wakosahihi kwakilajambo mbonawanajaribu kuwafunga midomo wapinzani nawakati ufisadi wore mkubwa uliotokea kwenye ichi hii sokuzanyuma uliibuliwa na hao wapinzani? Mimi sonahofu ns lisu hofu yangu iko kwa upande wapoli inamaana hawawezi kuongea mpaka wasikie wapinzani wanaongea? NNE he kunaukwelikwamba ichi imepigwa fine kwakukamata makinikia?nakama ndivyo mini tafsiri yake?

    ReplyDelete
  2. Wasahili wanasema kusoma sio kuelimika. Muheshimiwa Paul kagame wa Rwanda mwanzoni alpokuwa kwenye harakati zake za kuiweka sawa nchi yake alikuwa nao akina Lisu wengi tu waliokuwa wamedhamiria kumkwamisha lakini kagame ni mwanajeshi na sheria za jeshi ukimlea msaliti vitani kitachotokezea si kingine bali ni kupoteza vita. Kagame sio siri, kufanikiwa kwake kumechangiwa na kutokuwa na muhali na watu waliojaribu kumkwamisha na ikiwezekana aliwafuata wasaliti hata nje ya nchi yake . Huyu Lisu na wapuuzi wenzake wangelikuwa kule kwa kagame ingelibakia historia tu kuna mtu alikuwa anaitwa Lisu. Na la shangaza wakati mwengine utawasikia hao hao wapinzani wakiisifia Rwanda ooh Rwanda kijinchi kidogo kipo mbele kimaendeleo? Ukija katika suala la demokrasia kwa nchi za Africa hata ulaya basi Tanzania imepiga hatua kubwa. Mfano Marekani haitamruhusu muislamu kuwa kiongozi wao wa kiti cha urais. Vile Ville nchi kama uswisi. Tanzania haki sawa kwa wote uwe mweupe mweusi uwe na dini au usiwe nao mazali ni mtanzania na una sifa za uongozi hakuna kitakachokuzuia kupata nafasi. Na nadhani madhara ya Tanzania kuwa na demokrasia pana ndipo ilipozalisha viongozi wenye misimamo ya hovyo kupinga maendeleo huku wakiwadanganya watanzania wachache wenye maono finyu kuwa eti wao akina Tundu Lisu ni watetezi halisi wa nchi? Tundu Lisu na wafuasi wake kamwe hawawezi kuwa watetezi halisi wa watanzania bali siku zote watakuwa wasaliti na wanafiki wakubwa wenye nia mbaya sana kwa Tanzania. Lisu is the Eclipse face of trouble among of the Tanzanian society. Hata kule nchi za kipepari wanaojiita watetezi wa haki za binaadamu baada ya kukosa cha kutetea wakaanza kutetea usenge na usagaji hebu jiulize? haki ya binaadamu akizaliwa mwananamme haki yake ya msingi ni kuhakikisha kuwa anakuwa mwanamme inakuwaje unatokezea utetezi unaodai kanyimwa haki ya kuwa mwanamke? Na huko ndiko akina Tundu Lisu wanapotupeleka.
    Hongera sana mtoa mada hapo juu kwa uchambuzi wako wa kina kuhusu matabaka ya wasaliti inayokabiliana nao nchi yetu kwa kweli katika hii vita kwa kuwa Tanzania ni nchi ya kidemokrasia hatuwezi kuchukua hatua za kagame kukabiliana na wasaliti basi tunahitaji wasomi kama nyinyi kuwaelimisha watanzania tena tafadhali msichoke mpka kieleweke. Utaona hapo Lisu na kundi lake hapana shaka ni highly timokrasi people ever evolve in Tanzania .

    ReplyDelete
  3. Ndugu Muandishi.

    Kumbuka kuwa Tanzania ni nchi ya kidemocrasia (Japo ndogo) na kazi ya wapinzani ni kuikosoa Serikali sasa unaposema kina Tundu Lisu niOligaki uliitaka kina anachokifanya Raisi wetu wawe wanakishaabikia. Upinzani maana yake kutafuta kasoro za Serikali kutoa makosa hata kama baadhi yenu (wachache) mtaona yana manufaa au kuhofia kutumbuliwa au kupata cheo.
    Kwa mfano bomoabomoa inayoendelea inamaana ulitaka kina Tundu Lisu wanyanyue mikono kwa kufaraha walisherekee! Saa zingine uchama wekeni pembeni kama mnahisi kuna kosa elezenu wino wenu kutendea haki.
    Mfano mwengine wewe kwa maoni yako utauwita Arostrokasi wa kuzuia wapinzani wasifanye mikutano ya hadhara huoni hii ni sera ya kuuwa demograsia nchini? au Bunge kutoonyeshwa moja kwa moja hii nayo Timokrasi!
    kuipokonya Cuf Zanzibar Ushindi wake hii nayo Mwendo kasi!

    Acha zako Muandishi na utashi wa Chama chako.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Siyo kila kitu upinge kaka kuna vya kupinga siyo kwamba nchi imeingia kwenye majaribu harafu wewe unafurahi Nina umri Wa miaka 23..lakini upeo unatosha kuchambua mambo kuna vitu vya kupinga sawa lakini vingine kama watanzania tunapaswa kuungana pomoja kaka hawa wazungu hawana la maana ukiwapa na speed governor ndo umeisha kwa hiyo lissu ni mwanasheria anapaswa atuoneshe umahiri wake katika kada ya sheria asaidie nchi kuibiwa kisa sheria ,,,,,,ni hayo tu kwa hiyo lissu aungane na watanzania kutetea maslahi yao ila kama kuna kupinga siko huko kaka

      Delete
  4. Kuna dhana tunayotaka kuijenga watanzania ambayo Nadhani sio nzuri Kuwaita wale ambao hawakubaliani na yale tunayoyafikiria au kuyafanya Kuwa si wazalendo! Kama tulikubali kwamba nchi hii ni ya demokrasia basi hatuwezi kukwepa kukumbana na mawazo mengine. Hakuna mtu au Chama kinachoweza kutuhakikishia kwamba sera zake au mawazo take katika kila jambo ni zuri kwa asilimia Mia moja. Ujenzi wa nchi yeyote unachangamoto nyingi na Jin's I ya kuzitatua nayo ni changamoto ya ain't yake. Sasa tunapokuja kwenye Utashi wa kuzitatua hapo ndipo linapokuja la mawazo tofauti na hata Kuanza kuitana majina tofauti tofauti. Kuna mambo mengi mabaya yalifanyika kwenye nchi yet kwa makusudi na mengine kwa uzembe wetu tu. Sasa tunapotaka kutatua Haya makosa kila mtu anaweza asiwe na Imani na mwezake Lakini hili Halina Shaka kwamba tunajenga nchi moja na hivyo tuna mawazo tofauti na tutaendelea kuwa tofauti kwenye JinsI gani tutaijenga nchi

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad