Nisher: Adam Juma Anaweza Kufanya video Kali Hakuna Aliyechukua Crown Yake.

Nisher: Adam Juma Anaweza Kufanya video Kali Hakuna Aliyechukua Crown Yake.
Director Nisher amesema bado anashangazwa na watu ambao hadi leo wanadai yeye alikuja kuchukua taji (crown) ya Adam Juma katika music video industry Bongo kwani hakuna anayeweza kufanya hivyo.

Nisher amesema hayo alipokuwa akijibu maswali ya mashabiki wake waliyouliza kupitia mitandao ya kijamii, ambapo ameeleza kuwa hata sasa hivi Adam Juma anaweza kufanya video kali kwani hakuna aliyechukua crown yake.

“Mpaka leo kuna ambao wanasema mimi nilimfukuza Adam Juma kwenye music video industry, siwezi kumfukuza Adam Juma, nimekuta ana C.V yake ndefu inatisha, am respect him forever. Siwezi nikakaa nisema nimekuja kuichua crown Adam Juma na the game is big enough for the both side, industry ni kubwa kiasi kwamba inatutosha watu wote kila mtu anaweza kuwa na crown.

“Mimi na uwezo wa kunyamaza mwaka mmoja au miezi kadhaa nisitoe video lakini nikitoa video imetua, ni Nisher kwa sababu nishajenga hilo jina, nimelijenga zaidi ya miaka saba sasa, ipo nobody can take my crown, nobody can take Adam Juma crown,” amesema Nisher.

Pia ameongeza kuwa, “Adam Juma sasa hivi akiamua kupiga video inatoka kali, amerudi, so hakuna kukosea, hakuna kufeli. Biashara tu inakupanda na kushuka, kuna wakati ni high season na kuna wakati ni low season, its business,” amesisitiza
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad