Niyonzima Awajibu Wabaya Wake, Awaweka Roho Juu Yanga Ngao ya Jamii


Niyonzima Awajibu Wabaya Wake, Awaweka Roho Juu Yanga Ngao ya Jamii
Haruna Niyonzima ambaye ni mchezaji mpya wa klabu ya soka ya Simba SC aliyekuwa akicheza kwa mahasimu wao Yanga, amefunguka maneno ambayo yanaonekana ni kama madongo wa watu wanaomchukia kwa sasa.



Akiongea na waandishi wa habari baada ya kumalizika kwa mchezo wa kirafiki kati ya Simba na Rayon Sports ya Rwanda, mchezaji huyo amesema hakuwahi kuwa na ndoto za kuja kucheza Tanzania lakini mpira ndio kazi yake na kazi ni sehemu yoyote hachagui.

“Yanga wameumia na nini, wapenzi wa Haruna lakini mimi niseme yote ni maisha na mimi ni mchezaji wa mpira siwezi kujua nitaishia wapi lakini kikubwa ni kufanya kazi yangu. Pia nawashukuru Yanga ni timu ambayo mpaka sasa hivi nimecheza misimu mingi sana kuliko timu zote duniani, ni kitu cha kuwashukuru nimeishi nao vizuri mashabiki, wana Yanga, wapenzi wa Haruna ambao walikuwa wanampenda akiwa Yanga na watu wote ambao wameni support nikiwa Yanga,” amesema Niyonzima.

“Wamenionyesha ushirikiano lakini Mwenyezi Mungu anakuwa na mambo yake mengine, nimekuja Simba na ninaamini nimekuja kufanya kazi. Mimi niseme kuwa sikuwa na ndoto za kucheza Tanzania lakini Mwenyezi Mungu ndio anajua wapi mtu ataenda mimi sioni tatizo ni kitu tu cha kushukuru kwa sababu kila kitu kinapangwa na Mungu na hii ni kazi unajua kazi ni sehemu yoyote, mimi naomba Mwenyezi Mungu anibariki niweze kufanya kazi zangu vizuri tu basi,” ameongeza.

“Mimi naamini tukifanya kazi kwa ushirikiano tukawasikiliza walimu na sisi wenyewqe tukapendana kwa sababu tunawatu wenye experience ni watu wakubwa, watu wazima ambao tukiamua hatuwezi kukosa pointi tatu naamini tutakuja kufanya vizuri zaidi.”

Niyonzima amesisitiza kwa kusema kuwa anatamani kufunga goli katika mechi ya Ngao ya Jamii ambayo itachezwa August 23 mwaka huu katika uwanja wa Taifa ili aweze kuwaaga watu wa Yanga vizuri.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad