JESHI la Polisi katika Kaunti ya Siaya linaendelea na upelelezi baada ya mwili wa mwalimu wa kike aliyetambulika kwa jina la Caroline Odinga ambaye alikuwa msimamizi msaidizi wa Tume ya Uchaguzi (IEBC) katika Uchaguzi Mkuu wa Kenya wa Agosti 8 mwaka huu.
Mwili wa mwalimu huyo wa Ugenya High School ulikutwa katika soko la Sega jana Jumamosi asubuhi na watu waliokuwa wakielekea katika mazishi ya Mkurugenzi wa TEHAMA wa IEBC, Chris Msando, Kijiji cha Lifunga.
Mkuu wa Polisi katika Kaunti ya Siaya, Sarah Duncan amesema uchunguzi unaendelea na upelelezi wa awali unaonyesha kuwa marehemu alibakwa na watu wengi na sehemu zake za siri pamoja na sikio moja kukatwa vibaya.
Familia yake inaeleza kuwa mara ya mwisho alitoka nyumbani siku ya Ijumaa na kwenda kudai malipo yake kwa kazi aliyofanya ya usimamizi wa Uchaguzi Mkuu uliomalizika.
ODINGA Auawa, Mwili Wake Watupwa Sokoni inchini Kenya
3
August 20, 2017
Tags
Alafu kuna baadhi ya wazandiki wakitanzania wanausifia uchaguzi wa kenya na kusifia kuwa ushindi wa Uhuru kenyata ni wa kupigiwa mfano,jamani? Kenya watu tena muhimu wa tume ya uchaguzi wameuwawa na kuendelea kuuwawa na hapana shaka mikono ya serikali ya kenyata haiwezi kukosa kurowa damu na mauaji hayo sasa ni kipi cha kusifia hapo?
ReplyDeleteAlafu kuna baadhi ya wazandiki wakitanzania wanausifia uchaguzi wa kenya na kusifia kuwa ushindi wa Uhuru kenyata ni wa kupigiwa mfano,jamani? Kenya watu tena muhimu wa tume ya uchaguzi wameuwawa na kuendelea kuuwawa na hapana shaka mikono ya serikali ya kenyata haiwezi kukosa kurowa damu na mauaji hayo sasa ni kipi cha kusifia hapo?
ReplyDeleteHii ndo Demokrasia ya kweli. Wengi maraisi wa Africa wanarigi tu. Wengi watenda haki wanauawa. Siasa chafu zinamwisho. Wapenda madaraka wengi wanakasoro zao. Pesa, nguvu. Ubabe, Maringo. Wengi wao hawachaguliwi. Ebu fikiri mashine Ukaya, Watu wa mataifa ya nje wenye investments nchini wanachochea pea. Self interests Wamewekeza, wanaubia na maslahi ambayo wanataka bado yaendelee. Ni aibu sasa wamepata. Lumumba na kiingereza chake cha Uingereza, kama Barister na mbwembwe zake kashindwa. Hoja za upande wa mashtaka zilipangwa vizuri sana na kuonyeshwa moja kosa baada ya jingine. Waliprove mapungufu yaliyokuwepo wakati wa mchakato mzima wa kura. Hongera watu wa Kenya, mmetoa mfano wa kuigwa na Nchi zote za Africa.
ReplyDelete