Ofisi ya Waziri Mkuu Yaanzisha Programu Maalum kwa Vijana ili Kukuza Ujuzi Wao

Ofisi ya Waziri Mkuu Yaanzisha Programu Maalum kwa Vijana ili Kukuza Ujuzi Wao
Ofisi ya Waziri Mkuu imeanza programu maalum ya kukuza ujuzi kwa vijana katika kukabiliana na tatizo la ajira nchini.

Waziri wa Nchi katika Ofisi ys Waziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira, Kazi Vijana na Watu wenye ulemavu Jenista Mhagama amesema mara baada ya kupokea maandamano ya vijana kutoka mikoa mbalimbali  ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya vijana duniani.

Amesema vijana watakaohusika katika programu hiyo ni pamoja na wale wako katika maeneo ya kazi na wale waliomaliza elimu ya vyuo vikuu na kwamba vijana 13,400 walioko katika maeneo ya kazi watanufaika .

Amesema mafunzo hayo yatafanyika katika sekta mbalimbali ikiwemo miundombinu, kilimo, mifugo na viwanda vidogo vidogo nchini.

Kwa mujibu wa Jenista sensa ya mwaka 2012 inaonyesha kuwa watu wenye uwezo wa kufanya kazi ni milioni 25 kati ya milioni 44 na kwamba asilimia 56 wana umri kati ya 15 na 35 lakini asilimia 11.7 wameathirika na ukosefu wa ajira.

Maadhimisho hayo yanazishirikisha taasisi mbalimbali za umoja wa mataifa.




Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad