Unaweza kusema Qatar hawataki mchezo kuhusiana na Kombe la Dunia mwaka 2022.
Maana wametangaza ujenzi wa uwanja mpya utakaojulikana kwa la Al Thumama, yaani kibaragashia.
Mwonekano wa uwanja huo ni kama kibaragashia na utakuwa na uwezo wa kuchukua watu 40,000 lakini thamani yake ni pauni bilioni 5, hivyo kuufanya kuwa mmoja wa viwanja ghali duniani.
Umbo lake la 'gahfiya' yaani kofia aina ya kibaragashia ndiyo inaufanya kuwa kivutio zaidi.
Imeelezwa kama ilivyo viwanja linguine vilivyojengwa kwa ajili ya Kombe la Dunia, kutakuwa na mfumo wa kisasa wa AC ndani yake ili watu kupata hewa safi kwa kuwa kipindi hicho kutakuwa na joto kali nchini humo wakati wa Kombe la Dunia.
Ukiachana na Uwanja wa Al Thumama, kuna viwanja linguine saba vinaendelea kujengwa ukiachana na ule wa Khalifa International uliozinduliwa Mei, mwaka huu.