Raila Odinga Kufichua Madai ya Namna Alivyoibiwa Kura



Raila Odinga Kufichua Madai ya  Namna Alivyoibiwa Kura
Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga aliyeshindwa katika uchaguzi wa urais uliopita ameliambia gazeti la Financial Times nchini Uingereza kwamba atafichua ushahidi siku ya Jumanne kuhusu vile alivyoibiwa kura.

''Tutauonyesha ulimwengu ulivyochezewa'' .
Bwana Odinga ambaye alikuwa akiwania urais kwa mara ya nne pia alibaini kwamba hatowania tena urais na kwamba aliwataka Wakenya kujua kilichofanyika wakati wa uchaguzi huo.

''Sio swala la kuwa mbifansi, Sio swala kuhusu Raila Odinga, Sitawania urais tena......tunataka Wakenya kujua kile kilichofanyika, na kile ambacho ulimwengu haujui kinafanyika''.

Bwana Odinga amedai kwamba wadukuzi waliingilia kompyuta za tume ya Uchaguzi na kuweka hesabu ambazo zilimpatia ushindi rais Uhuru Kenyatta.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad