Rais John Magufuli Ampongeza Rais Mteule wa Kenya Uhuru Kenyatta...Soma Hapa Alichoandika

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli kupitia ukurasa wake wa Twitter, amempongeza Rais Uhuru Kenyatta kuchaguliwa kuiongoza Jamhuri ya Kenya kwa muhula mwingine wa miaka 5. Amemtakia mafanikio mema.

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (IEBC), Ndugu Wafula Chebukati usiku wa kuamkia leo alimtangaza Uhuru Kenyatta kuwa Mshindi wa kiti cha Urais baada ya kupata kura 8,203,290 sawa na asilimia 54.27 ya kura zote huku mpinzani wake aliyegombea kupitia Muungano wa Upinzani wa NASA Ndugu, Raila Odinga akipata kura 6,762,224 sawa na asilimia 44.74 ya kura zote.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad