Rais Magufuli Atoa MAAGIZO Mazito TAKUKURU

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amewataka viongozi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kutokuwa na kigugumizi cha kuchukua hatua pale wanapokuwa na ushahidi dhidi ya watu wanaojihusisha na vitendo vya rushwa.

Mhe. Rais Magufuli ametoa kauli hiyo  tarehe 28 Agosti, 2017 alipotembelea na kuzungumza na wafanyakazi wa TAKUKURU katika ofisi za makao makuu ya taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam.

“Kuna mambo mengi ya hovyo yanafanyika, tumehakiki pembejeo za ruzuku na kubaini madai ya Shilingi Bilioni 48 ni hewa, tumebaini wafanyakazi hewa zaidi ya 19,500, tumebaini kaya masikini hewa 56,000 zilizopaswa kupata fedha TASAF, tumebaini wanafunzi hewa 5,850 waliotakiwa kupata mkopo, kuna vichwa vya treni 11 vimeletwa bila kuwepo mkataba na mengine mengi, haya yote yanafanyika kwa rushwa, nataka kuwaona mnachukua hatua stahiki” amesema Mhe. Rais Magufuli.

Mhe. Rais Magufuli amesema ana imani na TAKUKURU na amewataka wafanyakazi wa taasisi hiyo kufanya kazi kwa kuzingatia weledi, uzalendo na uadilifu mkubwa na kwamba Serikali itafanyia kazi changamoto zinazowakabili.

Katika mkutano huo Mhe. Rais Magufuli amepokea masuala mbalimbali kutoka kwa wafanyakazi wa TAKUKURU na amewaahidi kuwa Serikali itayafanyia kazi ili kuboresha maslahi yao na mazingira ya kazi.

Mkutano huo umehudhuriwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Anjellah Kairuki, Katibu Mkuu Dkt. Laurian Ndumbaro na Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Bw. Valentino Mlowola.

Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi na wataalamu wanaosimamia utekelezaji wa miradi mikubwa ikiwemo ujenzi wa mradi wa umeme katika maporomoko ya mto Rufiji (Stieglers’ Gorge Hydropower Project), ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kisasa (Standard Gauge) na ujenzi wa barabara mbalimbali nchini, Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Katika Mkutano huo, Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medard Matogolo Kalemani ametoa taarifa ya maandalizi ya awali ya kuanza kwa ujenzi wa mradi wa umeme wa Stiegler’ Gorge na kwamba zabuni ya kuanza kwa ujenzi huo itatangazwa tarehe 30 Agosti, 2017.

Mhe. Rais Magufuli amesema fedha za kuanza kwa ujenzi wa mradi huo mkubwa utakaozalisha Megawatts 2,100 zitakazoingizwa katika gridi ya Taifa zipo.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam

28 Agosti, 2017
Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Jibu ni kwamba, CCM ni ileile. Watu wangapi wenye hutuma kubwa tu bado wapo huru. Wengi wao wakiwa viongozi wa juu CCM au walioteuliwa na CCM. Tulisema toka mwanzo, mfumo mzima ndani ya CCM ni uozo. Hakuna anayeadhibiwa. Kamatakamata kila siku, wanaachiwa huru. Wengine wakitetewa baadaye na wakuu wa juu ndani ya CCM. Sasa mtakomeshaje jambo kwa miaka zaidi ya ishirini wote bado mpo huru. Wote kwa namna hii au nyingine mmeshiriki kuletea Tanzania wizi, MMekuwa mafisadi wakuu, mmeuziana viwanda, majumba ya serikali, mmepitisha mali bandarini, mmejenga majumba ya kifahari kwa wizi au rushwa, mmepata magari kutoka kwa Wachina na wengine kujengewa nyumba na viwanda bure na mnavimiliki.
    Sasa mtamtumbua nani. Na mtaanzia wapi. Na utamchagua huyu na kumwacha yule kwa vipi. Huu ni mchezo unaojulikana kwa miaka mingi sana. Watu wanajua hii ni geresha tupu. Mbona unao akina Chenge na bado unafanya kazi nao. Wengine wamestaafu, je, Utadiriki kuwatumbua nao pia. Ni rahisi kusema hutaogopa viongozi wa dini au wa juu wa serikali mbona hatuoni haya yakitekelezwa. Basi watu wataendelea kuiba, wakijua utapiga kelele utawatoa kazi lakini wameshakuwa matajiri. Wanajua ukisimamia maneno unayoyasena, hakuna hata mtu mmoja kuanzia maraisi, mawaziri, Mapolisi, na Baaddi ya mapadre na Wanajeshi, hakuna atakayepona.Labda ujenge kwanza gereza la kifahari?
    Maneno matupu hayavunji mfupa.

    ReplyDelete
  2. Kweli kabisa CCM ndio ile ile lakini imejivua gamba na kuwatimuwa mafisadi makapi ili kiwatumikie watanzania kwa uadilifu zaidi. La kushangaza hivyo vyama vya upidhani na mashibiki wake kama vile wamerogwa kwani baada ya watanzania kuanza kuwaamini kidogo tu hafla wamekwenda kukumbatia mafisadi yaliokuwa yakipigiwa kelele na kulaaniwa kule CCM kuwa ndio chanzo cha uozo wa ufiasdi Tanzania. Ukimuona mtu anakula matapishi yake basi kama kuna kamba karibu mfungeni haraka kabla hajadhuru watu wengine kwani ni mgonjwa wa akili huyo. Chadema wamemtusi Lowasa. Walimchana chana kwa kila sifa ovu inamkabili bidanamu. Walimraruwa Sumaye kwa kila baya linalofaa kumtupia kiongozi muovu. lakini hii leo Sumaye na Lowasa ni viongozi mubashara wa Chadema. Kwa hivyo tunarejea tena pale pale ukimuona mtu anakula matapishi yake ni mgonjwa wa akili huyo si mzima. Tusishangae kuwaona akina Tundu Lisu wakiropokwa hovyo kama vile wamekunywa maji mabovu. Hakuna kama CCM kwa siasa za tanzania na itachukua muda kumpata mbadala wake. Na Maghuful sio bulldozer tena sasa hivi ni kifaru cha vita. Hao wanaojaribu kumsema kwa ubaya wengi wao ni wale waliokula matapishi yao si wazima wa akili. Bali kazi anazozifanya Maghuful ikiwa zimeonekana hadi na kina BillGate sasa wewe uliekuwa huna msaada wowote hata wa kujisaidia wewe mwenyewe endelea kupiga kelele na kukumbatia mafisadi makapi yaliyotapikwa na CCM

    ReplyDelete
  3. Ama kweli.. Wadau hapo juu wote mmekita na chuki za kisiasa.. Mh Raisi anazungumzia maendeleo na miundo mbinu kuboreshwa. nyinyi mnazungumzia CCM.
    Jamani hembu tujaribu kujiweka sawa sawa kichwaniMada inaeleweka ufuatiliaji na uwajibishaji ndicho kinachozungumzwa sasa haya mengine ya wakati wa Hewa yameshapitwa na kama kuingizwa katika ufisadi yameshatokea na mafisadi wengine wameihama hiyo CCM na wamekwenda upandw wa pili.
    Lakini hapo ndipo unaangalia Dharira na hatima ya huyu mtoto wetu Magu iko wapi. Ni mwenye uchungu na nchi yake. na sisi ni wa kushirikiana nae ili tufike huko runapo taka.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad