RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli ameamuru eneo la ekari 50 lililopo Mkata mkoani Tanga ambalo walipewa Mgambo JKT miaka saba iliyopita kwa ajili ya kujenga kiwanda na wakashindwa kuliendeleza, walirudishe haraka kwa serikali ya kijiji ili lipangiwe matumizi mengine.
Hayo ameyasema leo wakati akiwa njiani kuelekea Tanga kwa ajili ya kumpokea mgeni wake, Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda ambapo kesho wataweka jiwe la msingi la ujenzi wa mradi wa Bomba la Mafuta kutoka Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani Kaskazini mwa Tanga.
Rais Magufuli amekuwa akisisitiza kuwa wawekezaji au taasisi itakayopewa eneo kwa ajili ya kujenga kiwanda lazima ifanye hivyo, kushikilia eneo bila kuliendeleza kutasababisha mhusika anyang’anywe eneo hilo na apewe mwingine mwenye uwezo wa kuliendeleza.
Aidha rais ametoa onyo kwa viongozi waliohusika kuhujumu kwa kujinufaisha na fedha kiasi cha Tsh milioni 500 za ujenzi wa Hospitali ya Mkata kuwa wajiandae kuzirudisha ama kwenda gerezani.
RAIS Magufuli Sio wa Mchezo..Aamuru Mgambo Kurudisha Eneo la EKARI 50
2
August 03, 2017
Tags
Huu ndiyo Uadilifu. Tuliokiwa tunaulilia na kuutamani Miaka nenda Miaka ridi.. Mungu wameitikia maombi yetu na kutulrtea Mtoto wetu wenyewe mwenye uchungu na sisi. Hongera Baba na Hongera Wa Tanzania wote wenye kukuelewa na kutoa Ushirikiano na timu yake wote. Mungy akuweke JPJM
ReplyDeleteHuu ndio udikteta wenyewe!
ReplyDelete