Rapa Roma Mkatoliki amefunguka juu ya harakati ya kuingia Bungeni mwaka 2020 na kusema hiyo ni sehemu nzuri kwake kufunguka mambo mengi ambayo kwenye nyimbo zake huenda anashindwa kuyazungumza kutokana na kutokuwa na kinga.
Rapa Roma Mkatoliki akiwa na Mtangazaji wa kipindi cha NIRVANA, Deogratius Kithama.
Roma Mkatoliki amesema hayo kupitia kipindi cha NIRVANA kinachoruka kila Jumanne kuanzia saa tatu usiku kupitia ting'a namba moja kwa vijana EATV, alipokuwa akiongea na mtangazaji wa kipindi hicho Deogratius Kithama, Roma anakiri kwamba amekuwa akishauriwa sana kugombea Ubunge mwaka 2020 hivyo anadai ataangalia ingawa kwa mazingira anayoyaona yeye Bungeni ndiyo sehemu sahihi yeye kuongelea kero za wananchi.
Kwa Tanzania baadhi ya wasanii ambao walikuwa wakiimba ngoma zinazogusa maisha ya watu kila siku na kuwapigania watu kupitia tungo zao kama Joseph Mbilinyi na Profesa Jay waliweza kuaminiwa na wananchi na kupigiwa kura na sasa ni wabunge wanawakilisha wananchi kupitia chama cha upinzani bungeni, hivyo inawezekana Roma Mkatoliki anataka kufuata nyanyo zao kwani naye amekuwa akifanya harakati na kutetea wananchi kupitia tungo zake kama ambavyo wao walikuwa wakifanya.