RCO Awaonya Wachimbaji wa Madini Wanaotumia Mabomu ya Kienyeji
0
August 22, 2017
Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya jinai wa Mkoa wa Manyara (RCO) Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Joshua Mwafulambo amewataka wachimbaji wa madini wenye mabomu ya kienyeji kuacha tabia hizo.
Amesema hayo akiwa anawatuhumu wachimbaji wa madini ya Tanzanite wanaojihusisha na utengenezaji wa mabomu hayo akidai kwamba ni hatari kiusalama.
Amesema endapo kuna mchimbaji anajifahamu kumiliki mabomu hayo ajisalimishe mwenyewe kwenye kituo cha polisi Mirerani, kabla hatua kali za kisheria hawajachukuliwa.
Mwafulambo ameyasema hayo leo wakati akizungumza na wamiliki na mameneja wa migodi ya madini ya Tanzanite wa Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara.
Tags