RCO Awaonya Wachimbaji wa Madini Wanaotumia Mabomu ya Kienyeji


RCO Awaonya Wachimbaji wa Madini  Wanaotumia Mabomu ya Kienyeji
Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya jinai wa Mkoa wa Manyara (RCO) Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Joshua Mwafulambo amewataka wachimbaji wa madini  wenye mabomu ya kienyeji kuacha tabia hizo.

Amesema hayo akiwa anawatuhumu wachimbaji wa madini ya  Tanzanite wanaojihusisha na utengenezaji wa mabomu hayo akidai kwamba ni hatari kiusalama.

Amesema  endapo kuna mchimbaji anajifahamu kumiliki   mabomu hayo ajisalimishe  mwenyewe kwenye kituo cha polisi Mirerani, kabla hatua kali za kisheria hawajachukuliwa.

Mwafulambo ameyasema hayo leo wakati akizungumza na wamiliki na mameneja wa migodi ya madini ya Tanzanite wa Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad