Ripoti ya Mkemia Mkuu wa Serikali yathibitisha Manji Anatumia Dawa za Kulevya

Mfanyabiashara Maarufu nchini, Yusuph Manji akiteta jambo na Wakili wake, Hudson Ndusyepo wakati wakiwa ndani ya mahakama ya Hakimu Mkazi wa Kisutu jijini Dar es Salaam leo kabla ya kusomewa mashtaka yanayomkabiri.

SHAHIDI wa Kwanza katika kesi ya matumizi ya dawa za kulevya inayomkabili mfanyabiashara maarufu, Yusuph Manji amedai mahakani kuwa uchunguzi Wa mkemia Mkuu umeonyesha Manji anatumia dawa za kulevya.

Shahidi huyo wa kwanza wa upande wa jamuhuri, Ramadhani Kingai ambaye no Naibu Mkuu wa upelelezi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam amedai hayo leo mbele ya Hakimu Mfawidhi, Cyprian Mkeha Wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Akiongozwa na Wakili wa Jamhuri, Timon Vitalis, Kingai amedai, February 9 mwaka huu aliambiwa kufanya uchunguzi wa suala lililoripotiwa na Mkuu wa mkoa Wa Dar es Salaam Paul Makonda juu ya watuhumiwa wa dawa za kulevya wakiwemo Josephat Gwajima na Yusuph Manji.

Amesema alimuelekeza Dutektivu Koplo Sospter kuwapeleka Manji ambaye alifika katika kituo cha polisi mwenyewe na Gwajima kupelekwa kwa Mkemia Mkuu kupimwa juu ya tuhuma hizo za dawa za kulevya ambapo baadae walipata taarifa kuwa Manji anatumia dawa za kulevya.

Alidai baada ya ripoti hiyo, alielekeza Manji afunguliwe jalada la kutumia dawa za kulevya kisha kwa DPP ambaye alimfungulia mashtaka

Hata hivyo shahidi Kingai alipoulizwa nani alielekeza kuwa dawa anazodaiwa kutumia Manji ni Heroine alidai, yeye alifanya upelelezi tu ila anayeandaa mashtaka in DPP.

Naye shahidi wa pili Koplo Sospeter amedai alipokea maelekezo juu ya mtuhumiwa Manji ambapo moja ya maelekezo hayo yalikuwa yakimtaka kumpeleka Manji kwa mkemia Mkuu kwa ajili ya kupima sampuli ya mkojo ambapo baada ya kufuata taratibu za ofisi ya mkemia na kupata namba ya maabara alimpeleka Manji msalani ambapo aliweka mkojo kwenye chupa maalumu kwa ajili ya kufanyiwa vipimo.

Amedai Februari 10, mwaka huu majibu yalitoka na akakuta yanasema mkojo wake una chembechembe za dawa za kulevya.

Kesi hiyo itaendelea kesho.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. uongo kwa nini hamkuthibitisha wakati ule ule. why it takes time huo ni uonevu walio kamtwa ni wengi wale watumiaji wakasamehewa na wala hawajafungukiwa case bali baadhi walikaribishwa kwa bashite hio malininayo watoa roho ni jasho lao kutoka mababu zake na nyinyo chumeni sio kumdhulumu mtu na kufungia biashara zake baraka mutaipata wapi hii awamu hii apana aise shida na uonevu

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad