Wanajamvi salamu mbele!
Nimeona katika mtandao wa YouTube kile kinachoitwa kupatanishwa kwa Makonda na Ruge na mpatanishaji akiwa ni Rais John Pombe Magufuli. Naomba niweke maoni yangu hapa Jf na maoni haya yasitafsiriwe kuwa ninapinga watu kupatana wala kuishi kwa amani zaidi kushirikiana.
Makonda na Ruge wamekuwa katika mtanziko na hali ya kutokuelewana kwa muda wa miezi kadhaa sasa chanzo kikubwa kikiwa ni kile kinachodaiwa kwamba Makonda alivamia kituo cha utangazaji cha clouds tv na kupora vifaa kadhaa vya ofisi. Makonda alikwisha kanusha kuvamia clouds media katika kipindi chake alichojiandalia StarTv na kudai kwamba yote aliyoyaongea Ruge ni uongo ametunga akaenda mbali zaidi kusema Ruge hajui kitu zaidi ya utunzi wa story za mapenzi (kifupi msanii).
Wahenga wanasema mafahari wawili wagombanapo ziumiazo ni nyasi katika vita hii nyasi hazikukosekana. Mh Waziri Nape Mnauye ni mmojawapo katika juhudi za kutafuta ukweli na pengine suluhu la swala la Clouds media na Makonda yalimkuta ya kumkuta akaumia.
Kuna vyombo mbalimbali vya habari, watu binafsi na taasisi zingine ambazo kwa kweli zilisikitishwa na na kitendo cha Makonda kuvamia kituo cha Clouds media na wakatoa msaada wa kulaani na zaidi vilisusia kuandika habari za Makonda na mbali na vitisho vilivyotolewa na Rais ( refer "watch it")
Kubwa zaidi ni TEF (Jukwaa la Wahariri) lilisimama kidete katika hili kuhakikisha haki inatendeka kwa clouds media.
Jambo Kubwa la kunote wakati yote haya yanatokea mpatanishi (Rais Magufuli) aliamua kuegemea upande mmoja hii haijawahi kuwa sifa ya msuluhishi mahali popote pale duniani. Msuluhishi anatakiwa kuwa impartial asiyeegemea upande wowote.
Magufuli alikwishatamka hadharani kwamba kinachoendelea kwenye mitandao (tuhuma dhidi ya Makonda) ni udaku na yeye hasikilizi udaku. Hakuishia hapo alienda mbele zaidi na kutangaza interest kuwa hatamtumbua Makonda wala hata fanya lolote lile. Kauli kama hii inadhihirisha alikubaliana na alichokifanya Makonda na wala hakua akijali lolote na huku ni kuegemea upande mmoja.
Leo hii Mbele ya hadhara mlolongo huu wa matukio unamalizwa kwa kushikana mikono watu wawili yaani Ruge na Makonda? Kweli kabisa bila maelezo yoyote?
Mpaka naandika haya kuna mambo yameishughulisha akili yangu kama ifuatavyo.
Kwanza, Rais Magufuli katika mgogoro huu hakupaswa kuwa msuluhishi kwani alishaonesha upande hii inayofanywa ni danganya toto kwa Ruge.
Pili, swala hili lilipaswa sasa lisiwe mikononi mwa Clouds media na Ruge tena maana lilikwishafika kwenye chombo kinachohusika na vyombo vya habari TEF.
Tatu, Ni lazima umma uambiwe wanachopatana Ruge na Makonda ni nini ni ishu ya uvamizi au walikwaruzana mambo mengine barabarani? Na kama ni ishu ya uvamizi lazima tujue kwanza ukweli ni nani mkosaji ambaye anaomba radhi ili asamehewe? Je wanasameheana kwamba walikoseana Ruge alikosa nini na Makonda alikosa nini? Isijekuwa anayesamehewa ni Ruge kwa kumsingizia Makonda.
Je kuanzia sasa Clouds media wataanza kurusha habari za Makonda vipi kuhusu TEF na washirika wao?.
Vipi kuhusu Nape Mnauye? Na wengine walioumia kama nyasi remedy yao ni ipi?
Unless tupate maelezo kuwa kuna mazungumzo ya siri ya kuwapatanisha na mwenye makosa amefahamika na ameomba msamaha kilichofanyika ni kizungumkuti tu na kuuziana mbuzi kwenye gunia.
Zawadi B. Lupelo
Mpatanishaji Ni mpenzi WA mungu.
ReplyDeleteMtoa mada umeongea pumba. Hujui unachokiongea isipokuwa unachuki zako binafsi zilizojaa usiasa zaidi. Nape Mnawiwe nnaimani ameshaelewa kosa lake .kuna kitu kwa kimombo wanakita Chain of command katika uongozi. Mkuu wa mkoa au lets say state Governor or Regional commissioner what ever you wana call it. Ni kiongozi mwenye mamlaka mapana sana yanayohusiana moja kwa moja na kiongozi wa juu wa nchi. Huwezi kumtumbua makonda bila ya kumtumbua Maghuful na kwa taritibu za upatikanaji wa wakuu wa mikoa kwa nchi yetu ni kutoka kwa uteuzi wa raisi na vile vile ni raisi pekee ndie mwenye mamlaka ya kuwaajibisha zinapotokea hitilafu. Kwa nchi za wenzetu hasa zenye utaratibu wa kuwapata wakuu wa mikoa kwa njia za kupigiwa kura na wananchi wakuu wake wa mikoa wana nguvu zaidi wanauwezo wa kumvimbia hata raisi wa nchi katika maamuzi fulani wasioyaridhia. Ila utaratibu wa wakuu wa mikoa kuteuliwa na raisi kwa nchi kama Tanzania na Africa ni bora zaidi ili kuepusha utabaka na ukanda kujikita zaidi katika jamii. Nape alitakiwa kupata muongozo kutoka kwa muheshimiwa raisi na chama chake katika suala la Makonda badala ya yeye kufuata mihemko kutoka kwa wapinzani. Wapinzani hata Makonda akifanya vizuri wao watabeza tu sasa inapotokea Makonda kuteleza wapinzani hupata neno la kuisema vibaya serikali na bila kujitambua nape kama waziri alikosa busara au kama wanavyosema kugaiwa penzi kidogo na binti fulani kulimfanya atake kuthibitisha ushujaa zidi ya huyo dada lakini huu ni wakati wa Maghuful amini kama Makonda angekuwa si mtendaji mwenye kujitosheleza asingebaki pale. Uongozi wa mtu hupimwa kwa mapungufu na ufanisi wake na kama ufanisi unazidi mapungufu kwa asilimia kubwa yanini kumuadhibu kiongozi kama huyo ni vizuri kumrekebisha tu na nadhani hiyo ndio dhana halisi ya muheshimiwa raisi.
ReplyDeleteWewe ndiyo hata huelewi hata hii mada na unahitaji msaada. Aliyekwambia Nape aliunda tume ya kumtumbua Makonda ni nani?? hata uelewa wako nina u question, alichofanya Nape ni kuunda tume ya kutafuta ukweli wa kilichotokea pale CMG HQ. Mamlaka ya kutumbua au kutotumbua yanabaki palepale kwenye mamlaka yake ( Bashite) ya uteuzi.
DeleteKama ulimfuatilia Nape alisema "Taarifa tumeifikisha mamlaka zinazohusika kwaajili ya maamuzi"
Second, kwenye mada ya Zawadi maeneo yoote aliyoyagusa wewe umeona hilo moja tu la Nape??? kweli wewe umelogwa unhita kuombewa mapepo yakutoke, ume dwell kwenye eneo moja tuu, hata kuchambua mada nyepesi na iliyo wazi kama hii umeshindwa, kweli wewe huna tofauti na shoga yako Bashite. Pole sana dogo.