Tukio hilo lilitokea juzi jioni muda mfupi kabla ya matokeo ya uchaguzi wa TFF kutangazwa ambapo alionekana akilia nje ya ukumbi kutokana na kupata tetesi mapema za Mayay kushindwa katika kinyang’anyiro hicho mkoani Dodoma.
Mwamanda ambaye aliitumikia Yanga miaka ya nyuma akitokea Prisons ya Mbeya alipoulizwa sababu ya kutokea hicho alichokifanya alisema kuwa matokeo ya uchaguzi aliyapata mapema hivyo yalimuumiza roho hasa alipobaini kuwa Mayay ameshindwa.
Mwamanda amesema kuwa matokeo ya uchaguzi huo yalivuja na kumfikia kabla hata hatua ya kutangaza haijafika na kumfanya aumie baada ya kuonekana mgombea wake Ally Mayay ameshindwa.
"Nimeumia sana kusikia Mayay amepoteza uchaguzi huku watu wote wa mpira nao wakikosa nafasi zote hata zile za ujumbe hususani Julio (Jamhuri Kihwelo) aliyekuwa na sifa za wazi kupata nafasi hiyo.
"Mimi nilikuwa na nia ya kugombea ila kuna watu walinishauri na kuniambia niache kwani tayari walijua haya yatakuja kutokea, kwa kifupi mimi niwaambie tu mpira kama utaongozwa na watu wa kupangwa hatutapiga hatua yoyote hata siku moja," alisema.