Serikali Yaionya Kampuni Iliyosema Clouds FM Inaongoza Kusikilizwa Nchini Tanzania....


Siku chache tangu Kampuni ya GeoPoll ilipotoa takwimu za vituo vya redio na runinga vinavyosikilizwa na kutazamwa zaidi nchini, Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) imeingilia katika na kusema kuwa takwimu hizo ni batili.

Katika taarifa yake iliyotolewa leo Agosti 7, 2017, Ofisi ya Taifa ya Takwimu imesema kwamba takwimu hizo si rasmi kwa kuwa hukusanywa kwa mfumo ambao hautambuliki na NBS kwa mujibu wa kifungu cha 20 cha Sheria ya Takwimu ya mwaka 2015.

Siku chache zilizopita kampuni hiyo ilitoa takwimu zilizoonyesha kuwa Kituo cha Redio cha Clouds Fm ndicho ambacho husikilizwa zaidi nchini Tanzania huku kikifuatiwa na Radio Free Africa (RFA) na TBC Taifa.

Kwa upande wa vituo vya runinga, takwimu wa GeoPoll zilionyesha kuwa Clouds Tv ndiyo inaongoza kwa kutazamwa zaidi, huku ITV ikishika nafasi ya pili na kufuatiwa na East Africa Tv.

Kuona ripoti nzima ya GeoPoll kuhusu utazamwaji na usikilizwaji wa vyombo vya habari Tanzania bonyeza hapa

Katika taarifa ya Ofisi ya Takwimu hapa chini, wameitaka Kampuni hiyo kufuata taratibu zilizoanishwa katika Sheria ya Takwimu kwani takwimu zao za sasa hazijakidhi vigezo.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad