Serikali kupitia kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu Idara ya Habari, Zamaradi Kawawa imejibu hoja zilizotolewa na Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA Tundu Lissu kuhusu kushikiliwa kwa ndege ya Tanzania aina ya Bombadier Q-400 Dash 8 nchini Canada.
Zamaradi Kawawa amekiri kuwa ni kweli ununuzi wa ndege hizo umeingiliwa na mgogoro na kukiri kuwa ndege hiyo Q-400 Dash 8 inashikiliwa nchini Canada kwa madai ya kuwa ndege hiyo imeshikiliwa kwa mgogoro wa kutengeneza na wanasiasa wa Tanzania wasioitakia mema nchi ya Tanzania.
"Ununuzi wa ndege ya 3 ya Bombadier umeingiliwa na mgogoro uliotengenezwa na wanasiasa na watu wasioitakia mema Tanzania, Wanasiasa waliotengeneza mgogoro huo wanahujumu maendeleo ya nchi na usalama wa raia"- alisema Zamaradi Kawawa
Aidha Zamaradi Kawawa amesema kuwa ndege ya tatu ambayo ilikuwa inatarajiwa kuingia nchini mwezi Julai amedai kuwa itaingia muda si mrefu na kuwataka Watanzania waiamini serikali ya Tanzania iliyopo chini ya Rais John Pombe Magufuli
"Ndege ya 3 ya Bombadier ipo na inakuja kwahiyo wananchi waiamini Serikali yao ila serikali imesikitishwa na ushiriki wa wanasiasa na baadhi ya watu kuhujumu maendeleo ya nchi, Watanzania tuwe wazalendo kulinda, kutetea na kukabiliana na hujuma zozote zinazorudisha nyuma maendeleo ya Nchi, tuunge mkono jitihada za Rais Magufuli katika kuleta maendeleo bila kujali itikadi ya chama, kabila au dini" alisisitiza Zamaradi Kawawa
Mbali na hilo Kawawa amesema kuwa serikali imeanza kuchukua hatua kadhaa kuhusiana na mgogoro wa ununuzi wa ndege hizo
"Kuhusiana na mgogoro wa ununuzi wa ndege hatua za Kidiplomasia na sheria zimeanza kuchukuliwa ili kumaliza jambo hili" alisema Zamaradi Kawawa
Hapo Jana Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia Na maendeleo (CHADEMA) Tundu Lissu katika taarifa yake kwa vyombo vya habari alisema ndege hiyo imeshindwa kuwasili nchini kufuatia kesi ya madai iliyofunguliwa dhidi ya Serikali ya Tanzania nakupelekea kukamatwa kwa Ndege hiyo mali ya Tanazania.
Tunalilia hali ngumu ya maisha serikali imejibana imetumia fedha za wananchi kununua ndege kwa ajili ya kukuza uchumi wa nchi kupitia utalii na usafirishaji inatokea mtu kwa matakwa yake na utashi wake anaanzisha mgogoro wa kimasirahi wa ukuaji wa uchumi wa nchi yetu huyo anajiita mzalendo.
ReplyDeleteWe Mtafutaji,
ReplyDeleteUmeyazoa wapi hayo maneno. Unaamini vipi. Kama inamhusisha Lisu, si yeye aliyeamuru ndege ishikiliwe. Hivi Watanzania mbona hamna akili. Mtu anawaelimisha jinsi mambo yalivyotokea ili tujue nini kimetokea, uunaingiza siasa zisizo na mshikio. Alianza Zitto kuibua hii. Nyinyi watu badala ya kujielimisha mkajua sheria za kimataifa, na mikataba, unamvamia mtu binafsi anayekuelimisha. Ni ujinga kama huu wa elimu duni za kufukiri na kujisomesha ili tujue mambo sahihi na tushiriki sawa kwa utambuzi ambapo ni haki ya kila Mtanzania sababu ni pesa yako ya kodi unaamua kuwa mjinga. Na tumejaa wengi Wajinga nchini, tunatetea yasiyoeleweka sababu ya ujinga na upumbavu ambao tumeamua kuukumbatia kwa miaka mingi. Tukizidi kulalama bila mafanukio sababu ni Wajunga.Inaaibisha nchi.
Mimi napita tu
ReplyDelete