Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Nchini TUCTA Yaliamsha Dude, Ataka Waliofukuzwa Kwa Vyeti Feki Walipwe

Shirikisho la vyama vya wafanyakazi nchini TUCTA limeiomba serikali kuwapa mafao ambao walikuwa watumishi wa serikali na baadaye kuondolewa kwa kosa la kugushi vyeti ama kuwa na vyeti feki.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam leo Rais wa shirikisho hilo, Tumaini Nyamhokya  amesema kuwa mbali na watumishi hao kuwa na makosa ya kutumia vyeti feki lakini ni watumishi ambao waliweza kulitumikia taifa kwa uaminifu.

Katika hatua nyingine Rais wa shirikisho la amesema kuwa endapo kuna watumishi wa umma wanavyeti feki vinavyosomeka kama vya darasa la saba shirikisho litawachukuliwa hatua  kwa kuweka majina yao bayana na kuongeza kuwa waraka uliotolewa na wizara ya utumishi wa umma na utawala bora haujatoa ruhusa kwa wakurugenzi wa halmashauri na mashirika kuwaondoa kazini watumishi wenye vyeti feki vya darasa la saba.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad