Sifa 6 Unazotakiwa Kuwa Nazo Kuweza Kujiunga na Jeshi la Tanzania


Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) lilianzishwa tarehe 01 Septemba 1964 likiwa na lengo la kulinda uhuru wa nchi na mipaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mbali na lengo hilo, majukumu mengine ya msingi ya JWTZ ni pamoja na;

Kulinda Katiba na Uhuru wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Ulinzi wa Mipaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kufanya Mafunzo na Mazoezi ili kujiweka tayari Kivita wakati wote.
Kufundisha umma shughuli za Ulinzi wa Taifa.
Kushirikiana na Mamlaka za Kiraia katika kutoa misaada ya kibinadamu na uokoaji wakati wa maafa.
Kukuza elimu ya kujitegemea na uzalishaji kupitia Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).
Kushiriki katika shughuli za Ulinzi wa Amani Kimataifa.
Vijana wengi wamekuwa wakitamani kujiunga na JWTZ lakini hawajua njia sahihi wanazotakiwa kupitia ili kuweza kutimiza ndoto zao ambapo hali hiyo inapelekea kuwapo kwa matapeli wengi. Matapeli hao hutumia kigezo cha watu kutokujua namna ya kujiunga na JWTZ kuweza kuwatapeli wakisema kuwa wanaweza kuwasaidia.

Mbali na hilo, vijana hao wanakuwa pia hawafahamu sifa za mtu anayeweza kukubaliwa kujiunga na JWTZ. Wengi hukatishwa tamaa wakiamini kuwa hawana sifa za kufanya hivyo, na wengine kutapeliwa wakiahidiwa kusaidiwa kumbe hawana sifa za kujiunga na JWTZ.



Kuna sifa 6 kuu ambazo mtu yeyote atakayezitimiza anataweza kuandikishwa. Uandikishaji mtu huyo kujiunga na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa sifa zifuatazo:

Awe raia wa Tanzania
Awe na elimu ya kidato cha nne na kuendelea na awe amefaulu.
Awe hajaoa/hajaolewa
Awe na umri kuanzia miaka 18 hadi 25
Awe na tabia na mwenendo mzuri
Awe na akili timamu na afya nzuri
Masharti ya Utumishi Askari atapewa nambari ya utumishi baada ya kufaulu mafunzo ya awali. Atalitumikia Jeshi kwa kipindi cha mwanzo cha miaka sita, baada ya hapo atafanya kazi kwa mkataba wa miaka miwili miwili kwa kibali cha Mkuu wa Majeshi.

Maafisa Bodi ya Uteuzi wa Maafisa (Officers Selection Board) huwafanyia usaili Askari wenye elimu ya kidato cha sita na kuendelea toka Vikosini na Shule za Askari wapya (Recruitment Schools). Watakaofaulu masailiano hayo hupewa hadhi ya Afisa Mwanafunzi (Officer Cadet), na hupelekwa Chuoni (Tanzania Military Academy) kwa mafunzo ya Uafisa kwa muda wa mwaka mmoja.
Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Na je kwa wale wenye elimu ya ziada mfano nimesoma veta fani ya fitter mechanics na elim yangu ni darsa la saba hapo inakuje
    I

    ReplyDelete
  2. Na je kwa wale wenye elimu ya ziada mfano nimesoma veta fani ya fitter mechanics na elim yangu ni darsa la saba hapo inakuje
    I

    ReplyDelete
  3. Na je kwa wale wenye elimu ya ziada mfano nimesoma veta fani ya fitter mechanics na elim yangu ni darsa la saba hapo inakuje
    I

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad